Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Mtoto Runi Fabi(5) mkazi wa Kitongoji
cha Namleya,Ilembo,Kata ya Vwawa,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya amefariki
dunia baada ya kushambuliwa na kung'atwa na kundi la nyuki.
Tukio hilo limetokea Mei 27 mwaka huu majira ya saa sita mchana,wakati akicheza na watoto wenzake nje kidogo ya nyumba yao.
Balozi wa mtaa huo Bwana Hanzi Wega,
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha ya kwamba tukio hilo
ni la pili kutokea mtaani kwake.
Ameongeza kuwa mwezi Mei mwaka jana mwanamke marehemu Namyugumbi Nzunda, aliuawa baada ya kuvamiwa na kundi la nyuki.
Hata hivyo Baba mzazi wa mtoto huyo
Bwana Fabi Mjewa amesema alishangaa kuletewa mwanae...
NEW VIDEO:- CHRIS BEE - SIENDI MBALI
6 years ago