Pages


MTOTO AFUNGWA KAMBA YA KATANI MIGUU NA MAMA YAKE

Kamanga na Matukio | 05:15 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, MbeyaBi Rahabu Robert (26) mkazi wa mtaa wa Manga A, jijini Mbeya amekutwa amemfunga kamba ya katani kwenye meza mtoto wake wa kumzaa aitwaye Eliza Frank (4), kwa kile alichodai kuchoshwa na tabia mbaya ya uzurulaji. Tukio hilo limetokea Januari 25, mwaka huu nyumbani hapo majira ya saa 10 jioni na mtoto huyo kukutwa majira ya saa 12 jioni na majirani wakati mama huyo akiwa kanisani kwenye ibada. Baada ya majirani kubaini ukatili huo walimtaarifu Mwenyekiti wa mtaa Bi Rose Mwaisanga, ambapo naye alimfuata mama huyo kanisani katika Kanisa la Moravian Ruanda lililopo karibu na Hospitali ya K'S lililopo mtaa wa Mafiati. Wakati huo huo baada ya kufika nyumbani mama huyo...

UNYANYAAJI WA KIJINSIA:- MWANAMKE APIGWA , AFUNGIWA SIKU TATU NDANI BILA KUPEWA MATIBABU - MBEYA

Kamanga na Matukio | 04:49 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, MbeyaBi Judith Mnyape (32) mkazi wa Ghana Magharibi jijini Mbeya amepingwa na mumewe Bwana Clemence Luhimbo (36), maarufu kwa jina la Kidevuna kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kile kilichodaiwa na kuwa ni wivu wa kimapenzi. Tukio hilo limetokea Januari 14, mwaka huu majira ya saa 2 usiku nyumbani kwake ambapo mume alimpiga mkewe kwa kwa kutumia ufagio hadi kuvunjika hali iliyompelekea mwanamke huyo kupata majeraha na kisha kulazwa katika hospitali ya Rufaa jijini Mbeya Januari 20 hadi 21 mwaka huu. Mbali ya kumpiga mkewe Bwana Luhimbo, maarufu kwa jina la Kidevu ambaye ni dereva wa taksi anayeegesha kituo cha Baa ya Kalembo iliyopo Sokomatola, alimfungia...

MWANAMKE APANDISHWA KIZIMBANI KWA KOSA LA KUMUUA MWANAE - MBEYA

Kamanga na Matukio | 04:27 | 0 comments
Habari na Mwandishi wetuNeema Edson mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Namtanga Swaya jijini Mbeya amefikishwa katika mahakama ya mkoa kwa kosa la kumuua mtoto wake akiwa mchanga. Akisoma shitaka hilo mbele ya hakimu mkazi mfawizi Monika Ndyekobola mwanasheria wa serikari Ema Msofe amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo January 3 mwaka huu maeneo ya namtanga jijini hapa. Amemtaja mtoto aliyeuawa kuwa Steven Chinga ambaye alikuwa na umri chini ya miezi kumi na miwili kinyume na kifungu cha sheria namba 199 sura ya 16 kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Hata hivyo mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na dhamana ya kusikiliza kesi...

MGOMO WA MADAKTARI HOSPITALI YA RUFAA, MBEYA NINI TAMATI YAKE?

Kamanga na Matukio | 04:26 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, MbeyaMgomo wa madakta Hospitali ya Rufaa, Mbeya umeendelea huku madaktari hao wakidai kuwa mgomo huo utakuwa endelevu hadi hapo Serikali itakapo tekeleza madai yao. Katika mgomo huo madaktari hao wamesema mgomo wao umelenga kuishinikiza Serikali kuboresha huduma za afya, kuowaongezea mshahara, posho na malipo ya kazi hatarishi pamoja na kuwapatia makazi kama ambavyo sheria ya nchi inavyoelekeza. Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dokta Eliuta Sanker amesema mgomo huo umefanywa na madaktari wanafunzi 65 na madaktari wapya 10. Mgomo huo wa madaktari ulianza January 23 mwaka huu baada ya mwenyekiti wa kamati...

MAUAJI YA KUTISHA DHIDI YA WATOTO WAWILI MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:12 | 0 comments
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nsenga jijini Mbeya wakitoka kushuhudia mwili wa mwanafunzi mwenzao wa darasa la Kwanza Silvia Isaya (5) alieuawa kisha viungo vya mwili wake kunyofolewa ulimi, jicho la upande wa kushoto, sehemu za siri na mguu wake wa kushoto kuvunjwa. Baadhi ya wananchi wa Nsenga jijini Mbeya wakishuhudia mwili wa mwanafunzi wa darasa la Kwanza Silvia Isaya (5) alieuawa kisha viungo vya mwili wake kunyofolewa ulimi, jicho...

WANAWAKE WA KANISA LA MORAVIAN JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI WAPEWA MSAADA WA MAJIKO NA TAA AMBAZO HUTUMIA MIOZI YA JUA

Kamanga na Matukio | 05:33 | 0 comments
 Idara ya Wanawake na watoto Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi Tanzania limepokea misaada mbalimbali ikiwemo ya taa na jiko ambavyo vinazotumia miozi ya jua, ambapo msaada huo umetolewa na Kanisa la Moravian Ujerumani kwa ajili ya kuiwezesha idara hiyo kujikomboa kiuchumi. Jiko linalotumia miozi ya jua lenye thamani ya shilingi laki 5, lililotolewa na Kanisa la Moravian Ujerumani kwa ajili ya kuiwezesha Idara ya Wanawake na watoto...

WATOTO YATIMA WASAIDIWA WILAYANI CHUNYA - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:15 | 0 comments
 Waumini wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wakipokea msaada hivi karibuni kutoka kwa Bi Sandra Witschi raia wa Uswisi, anayefanya kazi katika Jimbo hilo katika Idara ya Watoto na Wanawake. Bi Sandra Witschi akisisitiza watanzania kusaidia watoto yatima na kwamba watoto hao wakiendelezwa kielimu, nchi itaondokana na wimbi la ongezeko la watoto wa mitaani. Bi Sandra akiwa katika picha...

WANANCHI WAONYWA KUACHA MARA MOJA KUTUMIA VIPODOZI HATARISHI.

Kamanga na Matukio | 02:35 | 0 comments
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bwana Paul Sonda, katika mkutano mkuu wa madaktari wa Hospitali na zahanati binafsi katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Youth Centre  wa Roman Catholic jijini Mbeya. Mmoja kati ya madaktari waliohudhurua mkutano huo akivitambua baadhi ya vipodozi hatarishi na madhara yake, katika mkutano mkuu wa madaktari wa Hospitali na zahanati binafsi katika mkutano...

MLINZI MBARONI KWA KUIBA SILAHA - MBEYA

Kamanga na Matukio | 01:41 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, MbeyaJeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia Devid John mwenye umri wa miaka 36 mfanyakazi wa Kampuni ya ulinzi ya Simike kwa tuhuma za kuhusika na wizi.Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amesema mtuhumiwa huyo pamoja na wenzake wawili, Herman Davidi na Eriki Ismaili, wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya Kirumo  Security waliiba bunduki aina ya Shotigun Green yenye namba 565650 ambayo ni mali ya kampuni ya Kirumo.Aidha Kamanda Nyombi ameongeza kuwa upelelezi zaidi kuhusiana na tukio hilo bado unaendelea....

WIMBI LA UBAKAJI LAZIDI KUSHAMIRI MKOANI MBEYA KIKONGWE ABAKA. - MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:15 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.Wimbi la ubakaji mkoani Mbeya limeendelea kushika kasi baada ya Mzee mwingine aliyefahamika kwa jina la Frank Mwakyeja (60 - 65), mkazi wa mtaa wa Ilolo B kata ya Isanga jijini Mbeya kuwabaka watoto wawili wa rika tofauti.Tukio hilo limetokea Desemba 5, mwaka uliopita ambapo aliwabaka watoto hao wa jirani yake mmoja akiwa mwanafunzi wa Shule ya msingi Manga, jijini hapa mwenye umri wa miaka 9 na mwingine mwanafunzi wa shule ya msingi Madaraka jijini hapa mwenye umri wa miaka 7 (majina yao yanahifadhiwa).Akizungumza na Mtandao huu Baba wa mmoja wa watoto walitendewa ukatili huo Bwana Gwakisa Mwakihaba (38), alifungua jarada la mashitaka MWJ/RB/270/2011, mnamo...

HOSPITALI NA ZAHANATI BINAFSI ZIMEASWA KUTOTUMIA DAWA ZA SERIKALI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:14 | 0 comments
Mganga mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya Dokta Seif Mhina, akizungumza na madaktari wa Hospitali na Zahanati binafsi katika Ukumbi wa Youth Centre uliopo katika Jiji la Mbeya.*****Habari na Ezekiel Kamanga, MbeyaHospitali binafsi zilizopo mkoani Mbeya zimeaswa kutotumia dawa za Serikali katika zahanati na hospitali ili kuepuka kufungiwa.Hayo yamesemwa na Dokta Reinfredy Chombo wakati akitoa maada katika ukumbi wa youth centre jijini mbeya alipokutana...

WILAYA YA MBEYA YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MADARASA.

Kamanga na Matukio | 06:02 | 0 comments
Habari na Mtandao huu, Mbeya.Wilaya ya Mbeya inakabiliwa na upungufu wa madarasa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2012. Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mbeya Evans Balama wakati akizungumza na bomba fm mwishoni mwa juma,balama amesema jiji la mbeya linakabiliwa na upungufu wa madarasa 59 wakati wilaya ya mbeya vijijini inakabiliwa na upungufu wa madarasa kumi na tano Aidha Balama ameongeza kuwa wazazi wanawajibu wa kukamilisha madarasa hayo ili wanafunzi waweze kuanza masomo haraka iwezekanavyo ili ifikapo mwishoni mwa mwezi february madarasa hayo yawe yamekamilika ili wanafunzi waanze masomo haraka Kwa upande wake afisa elimu mkoa...

KAMATI NDOGO YAUNDWA KUHAMASISHWA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF WILAYANI RUNGWE - MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:00 | 0 comments
Habari na Mtandao huu, Mbeya.Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imeunda kamati ndogo ya watu 10 itakayoandaa mikakati ya kuhakikisha hamasa ya mfuko wa afya ya jamii CHF inatolewa kwa wananchi ili waweze kujiunga kwa wingi.Kamati hiyo imeundwa na mkuu wa wilaya Jackson Msome aliyekubaliana na wadau wengine waliohudhuria mkutano wa wakuu wa Idara za halmashauri hiyo wa kupata taarifa za maendeleo ya CHF na pia kujadili mradi mpya wa kuwasaidia wanawake wajawazito wasio na uwezo kupata huduma za matibabu chini ya utaratibu wa mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF.Msome amesema ili kuhamasisha wananchi kujiunga kwa wingi ni lazima mikakati madhubuti iwekwe ikiwemo utoaji elimu kwa wakazi juu ya kuwa na...

MTU MMOJA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA UBAKAJI

Kamanga na Matukio | 05:57 | 0 comments
Habari na Mtandao huu, Mbeya.Robert John Hasani mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Majengo jijini Mbeya amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mbeya kwa kosa la ubakaji.Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Monika Ndyekobora mwanasheria wa Serikali Fransisi Rojasi amesema disemba 25 mwaka jana mshatakiwa alimbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 36 kinyume na kifungu cha sheria namba 130 B na kifungo 131 sura ya kwanza ya marekebisho ya mwaka 2002.Mstakakiwa amerudishwa rumande kwa kutokidhi masherti ya dhamana ambapo dhamana ni shilingi milioni mbili na kwamba kesi hiyo itasomwa tena Februari pili mwaka huu.Siku hiyo hiyo Eva Mwakibinga mwenye umri wa miaka...

KILA KUKICHA VITENDO VYA UBAKAJI VYAZIDI KULITIKISA JIJI LA MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:49 | 0 comments
Habari na mwandishi wetu.Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Jamesi mwenye umri wa miaka 40 amenusurika kifo baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali akituhumiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 16 makazi wa kata ya Ilemi jijini Mbeya. Tukio hilo limetokea jana majira ya saa mbili za asubuhi ambapo mtuhumiwa huyo aliingia nyumbani anakoishi binti huyo wakati akiwa peke yake na kuanza kumuingilia kimwili bila ridhaa ya mwanamke huyo. Wakazi wa eneo hilo walipata taarifa ya kubakwa kwa binti huyo baada ya kusikia kelele zikitoka ndani ya nyumba na kwamba baada ya kufika walimkuta kijana huyo akimwingia kimwili binti huyo ambAye tumemuhifadhi jina kwa sababua za kimaadili. Mama mzazi...

KIKONGWE MBAKAJI AFIKISHWA MAHAKAMANI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:47 | 0 comments
 Baba mzazi wa binti aliyebakwa na Mzee Asangile Kihaka (70), anayefahamika kwa jina la Bwana Ekson Nazareth  (47), ambaye pia ni mzee wa baraza mahakama ya Mwanzo ya Mbeya Mjini..  Mmoja wa wananchi wa eneo la Ghana akilaani vikali kitendo cha Mzee Asangile Kihaka (78) kumbaka binti wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la 7 katika Shule ya Msingi Mbata, ambapo ni tukio la tatu la mzee huyo kutenda.******Habari na Ezekiel Kamanga,...

RAIA 27 WA SOMALIA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI KINYUME NA SHERIA - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:41 | 0 comments
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi.***** Habari na Mwandishi wetu. Raia 27 wa Somalia wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha Sheria. Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema kuwa raia hao wa kigeni wamekamatwa jana maeneo ya Nonde jijini hapa wakati polisi wakiwa katika doria. Amesema kati ya raia hao mmoja ndiye aliyeweza kujitambulisha...

NYETI ZA MWANAMKE ZATOWEKA USINGIZINI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:32 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, MbeyaTunkumbukege Mbalaswa (20) mama wa watoto wanne mkazi wa kijiji cha Nsongola kata ya Bujela wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya amekuwa kwenye wasiwasi baada ya sehemu zake za siri kutoweka usiku wa Desemba 30 mwaka uliopita. Akiongea kwa masikitiko Bi  Tunkumbukege amesema alijifungua salama kabisa mtoto wa kiume October 2011 aitwaye Shaban Elia na hakupatwa na tatizo lolote hadi Desemba 30, mwaka jana alipokutwa na tatizo la sehemu za siri zikiwa zimeondolewa hali iliyomsababishia maumivu makali na hivyo kumlazimu kwenda Zahanati ya Bujela na kuonana na Daktari wa zahanati hiyo na kumpata dawa mama huyo akidai ni ugonjwa wa Fistula. Baada ya siku saba za matibabu...

WIMBI LA UBAKAJI MAUAJI:- WATU WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MATUKIO MAWILI TOFAUTI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 07:00 | 0 comments
Habari na Mwandishi wetu.John Jackson mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Mbeya Pick amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mbeya kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 12 maeneo ya Mbeya Pick. Akisoma shtaka hilo mwanasheria wa Serikali Faraja Msuya mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Monica Ndyekobora amesema mshtakiwa alimbaka mtoto huyo disemba 21 mwaka jana katika maeneo ya Mbeya Pick. Amesema kuwa kitendo hicho ni kinyume cha kifungu cha Sheria namba 130 kifungu cha pili E na kifungu cha 131 sura ya 16 marekebisho ya mwaka 2002. Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi January 31 mwaka huu na mtuhumiwa amerudishwa rumande kwa kukosa dhamana. Wakati...

MGOGORO KATI YA WAKULIMA, WANAKIJIJI NA MWEKEZAJI HALI NI TETE - MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:57 | 0 comments
Mfugaji Bwana Mungo Makubi (27) kushoto na Singu Mwakami (23) wakimtazama ng'ombe aliyeuawa kwa kugongwa na gari aina ya Toyota Landcruiser  lenye nambari ya usajili T 566 BQH. iliyokuwa ikiendeshwa na mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein baada ya kuwakosa wafugaji hao baada ya kujistiri nyuma ya mti na kisha hasira za mwekezaji kuishia kwa kumgonga ng'ombe huyo mwenye thamani ya shilingi...

WAZIRI MAGHEMBE - SIWEZI KUPINGA UAMUZI WA VIONGOZI WA MKOA KUZUIA UUNZWAJI WA KAHAWA MBIVU.

Kamanga na Matukio | 06:55 | 0 comments
Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe.****** Habari na Mwandishi wetu.Waziri wa kilimo chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe amesema kuwa hawezi kupinga maamuzi ya viongozi wa wilaya za Mbeya, Ileje, Rungwe na Mbozi kuhusu uamuzi wa kupinga biashara ya uuzaji wa Kahawa Mbivu.  Amesema kuwa hawezikutengua kanuni za Wizara na Bodi ya kahawa juu ya ununuzi wa kahawa mbivu na kuitaka Serikali mkoani Mbeya kusimamia...

CHAMA CHA MASOKO MKOANI MBEYA KIMEUTAKA UONGOZI WA HALMASHAURI YA JIJI KUTOWANYANYASA WAFANYABIASHARA.

Kamanga na Matukio | 06:44 | 0 comments
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama(kushoto) akiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbeya maarufu kama Ndomboro, katika moja ya vikao vya kujadili masuala mbalimbali ya kutatua kero za wakulima .(Picha na Maktaba yetu)******Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.Chama cha wafanyabiashara wa masoko jijini Mbeya kimeutaka uongozi wa Halmashauri ya jiji kutowanyanyasa wafanyabiashra hao kutokana na viongozi wa jiji kupandisha ushuru kiholela bila makubaliano...

MGOMO WA MADEREVA WA MALORI WAENDELEA - TUNDUMA

Kamanga na Matukio | 06:05 | 0 comments
Katikati mwenye koti jeusi diwani wa kata ya Tunduma Mheshimiwa Frank Mwakajoka Baada ya wafanyabiashara kushindwa kufanyabiashara zao na kupelekea kufunga kutokana na vurugu zilizotokea za kupingwa ucheleweshaji wa matokea ya uchaguzi nchini Zambia sasa ni shwari na wananchi wameanza kuvuka mpaka na wafanyabiashara kurejea katika shughuli zao.  Madereva wakielekea kukamilisha ushuru wa forodha na kukamilisha taratibu za kuvuka mpaka kuelekea...

KABURI LAFUKULIWA BAADA YA POLISI KURUHUSU KUZIKA KWA TUHUMA ZA WIZI.

Kamanga na Matukio | 05:38 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi.Jeshi la polisi mkoani Mbeya limeingia lawamani baada ya wananchi mbalimbali kulalamikia utendaji kazi wa Jeshi hilo baada ya kukumbatia vitendo vya kihalifu vinavyofanywa wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya, kutokana na kukinzana na dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi. Mnamo Januari 15, mwaka huu siku ya Jumapili, Jeshi la polisi kutoka Kituo cha Mlowo wilayani Mbozi walilazimishwa kufukua kaburi la kijana mkazi wa Msiha aliyeuawa hivi karibuni kwa tuhuma za wizi wa debe moja la karanga mali ya Sengo, katika kitongoji cha Nyelya, kijiji cha Hatelele na kisha kuchomwa moto na kuzikwa bila ndugu zake kufahamu, huku jeshi hilo likishindwa kuwakamata waliohusika...

WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SOWETO JIJINI MBEYA WASITISHA MGOMO

Kamanga na Matukio | 05:11 | 0 comments
Taswira ya baadhi ya vibanda na bidhaa ya nyanya katika Soko la Soweto Jijini Mbeya.*******Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.Wafanyabiashara wa soko la Soweto Mbeya wamesitisha mgomo baada ya kuafikiana na halmashauri ya jiji la Mbeya kuhusu kupunguza ushuru wa biashara. Mgomo wa wafanyabishara hao ulianza leo hii majira ya saa moja za asubuhi na ulidumu kwa muda wa masaa matatu, hata hivyo majira ya saa 4 za asubuhi wafanyabiashara hao...

WAZIRI MAGHEMBE ZIARANI MBEYA AKUTANA NA WAKULIMA WA ZAO LA KAHAWA - MBOZI

Kamanga na Matukio | 05:01 | 0 comments
 Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe.*****Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe leo hii amekutana na wakulima wa zao la kahawa kutoka wilaya za Mbeya, Mbozi, Rungwe na Ileje kwa ajili ya kujadili mstakabali wa zao la kahawa. Akiwa wilayani Mbozi, baadhi ya wakulima wa zao la Kahawa ambao walizuiwa kuhudhuria mkutano huo waliusimamisha msafara wa waziri...
Pages (14)1234567 Next
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger