Pages


Share to TwitterShare to Facebook WATANZANIA WATAKIWA KUWA WABUNIFU KATIKA UFANYAJI KAZI KWA BIDII.

Kamanga na Matukio | 01:11 | 0 comments
Na Esther Macha, Mbeya WATANZANIA wametakiwa kuacha kumtafuta mchawi wa hali duni ya maisha yao na kulalamika hali duni ya maisha na badala yake wawe wabunifu,wajitathmini na kufanyakazi kwa bidii na maarifa ili waweze kujipatia kipato na maendeleo ya familia,jamii na taifa kwa ujumla. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw.Abbas Kandoro wakati akifungua mkutano wa mashauriano juu ya malengo nane ya melania katika ukumbi...

MBUNGE AWASIHI WANACHAMA WA CHADEMA KUTOINGILIA MKUTANO WA CCM JIJINI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 01:10 | 0 comments
 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini mheshimiwa Joseph Mbilinyi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADE,A) akiwa juu ya gari lake, akiwasihi wakereketwa wa chama hicho kutoingilia Mkutano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), uliofanyika eneo la Stendi ya daladala ya Kabwe Jijini Mbeya.  Taswira kamili ya Mbunge akizungumza na wanachama wa CHADEMA  Taswira kamili ya hatua waliyokuwa wameifikia wanachama wa CHADEMA...

DAKTARI WA RUFAA MBEYA ATIWA MBARONI KWA MADAI YA KUPOKEA RUSHWA

Kamanga na Matukio | 01:09 | 0 comments
DAKTARI wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa Mbeya,Paul Kisabi (32), anayetuhumiwa kwa kupokea rushwa ya sh 200,000 Brandy Nelson,  Mbeya DAKTARI  wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Paul Ngiga amefikishwa katika mahakama ya Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kushawishi na kupokea Rushwa ya sh. 200,000 kutoka kwa ndugu wa mgonjwa. Akisoma mashitaka mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoa Mbeya Francis Keshenye Nimrodi...

PICHA YA MLINZI ALIYEUAWA KIKATILI.

Kamanga na Matukio | 01:41 | 0 comments
Mlinzi binafsi Simon Mwambene(45) Mkazi wa Kijiji cha Matula, Mbozi Mission Kata ya Magamba Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya, ameuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi alipokuwa lindo Desemba 13 mwaka huu majira ya saa 8:15 usiku alipokuwa analinda maduka 9 yaliyopo kijijini hapo yanayomilikiwa na Bwqana Frank Tenson, Mgala, Tweve, Sosten Kibona, Raphael Kisunga, Kamika Simbeye, Crispin Ndabila, Gody Mahenge, Anthon Mwazembe na Samwel...

PICHA YA KIUMBE WA AJABU ALIYEZALIWA MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 01:28 | 0 comments
Kiumbe wa ajabu azaliwa Mbeya, Viungo vyake vyazua gumzo macho yake yako katikati ya paji la Uso akosa Pua ila ana mdomo..!!!  Mama aliyejifungua kiumbe wa ajabu Bi. Melina Wilson mwenye umri wa miaka 17. Baba mzazi wa kiumbe wa ajabu Bwana Emmanuel Mbukwa mwenye umri wa miaka 24.(Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya...

WANAWAKE WATAKIWA KUWA NA DAFTARI LA KUMBUKUMBU LA BIASHARA,

Kamanga na Matukio | 01:27 | 0 comments
Na Ester Macha.  WANAWAKE Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya wametakiwa kuwa na daftari la kumbu kumbu  la biashara ambazo wanazifanya kila siku  ili liweze kuwapa tathimini  ya biashara wanazofanya ambayo itawasaidia kusonga mbele kimaisha na kuachana na dhana ya kuwa tegemezi kwa waume zao. Imeelezwa kuwa baadhi ya wanawake wamekuwa wakishindwa kuwa na tathimini nzuri nzuri ya fedha zao za biashara kutokana na kuwa na nidhamu mbaya ya matumizi ya fedha wanazozipata katika biashara zao. Kauli hiyo imetolewa jana wakati wa Kongamano la mwanamke jitambue   lilofanyika katika ukumbi wa Chinga Wilayani Mbarali ,na Mwakilishi wa Shirika la Elimisha...

Share to TwitterShare to Facebook WAZAZI BADO WAENDELEA NA DHANA YA KUWAFICHA WATOTO WALEMAVU MAJUMBANI MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 01:26 | 0 comments
Na Esther Macha, Chunya  SERIKALI Wilayani Chunya Mkoani Mbeya imewataka watumishi wa serikali kuacha kujihusisha na masuala ya siasa kama watendaji  kwani wanachangia kuleta vurugu ndani ya wilaya badala yake wajikite kutatua kero za wananchi. Kauli hiyo imetolewa jana  na Mkuu wa Wilaya ya Chunya ,Bw.Deodatusi Kinawiro wakati akitoa taarifa ya serikali katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri uliopo Wilayani humo. Bw.Kinawiro alisema  kuwa  kazi kubwa ambayo wanatakiwa kuifanya watumishi wa serikali ni kuangalia hali ya usalama ndani ya wilaya na kutatua kero za wananchi ambazo zinawakabili ,suala la siasa lina...

WALIMU WANAOJIHUSISHA KIMAPENZI NA WANAFUNZI KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

Kamanga na Matukio | 01:25 | 0 comments
SERIKALI wilayani Mbarali Mkoani Mbeya imesema itawafikisha katika vyombo vya sheria walimu wote wanaojihusisha kimapenzi na wanafunzi, huku baadhi yao wakiwapa mimba na kuwageuza wake zao watoto hao wa shule. Amesema  kuwa tabia hiyo ni uvunjaji wa maadili, na tabia ya kujihusisha kimapenzi na wanafunzi ni moja ya ubakaji kwa kuwa umri wa wanafunzi hao upo chini ya uangalizi wa walezi au wazazi. Kauli hiyo imetolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Bw. Hussein Kiffu   wakati wa mkutano wa wadau wa elimu uliofanyika wilayani hapa katika ukumbi wa Rutheran . Aliwataka walimu wenye tabia hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani ataanza kupita katika maeneo ili kupata taarifa...

CCM MBARALI YACHARUKIA VIONGOZI WASIOWAJIBIKA.

Kamanga na Matukio | 02:16 | 0 comments
Mwnyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Bwana Mathayo Lauren Mwangomo, amesema kuwa wakati wakubezwa kwa chama hicho kwa sasa haupo  kutokana na kujisogeza kwa wananchi ili kupata changamoto zao.  Ameyasema hayo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 17 mwaka huu katika Kijiji cha Ruiwa wilayani humo. Bwana Mwangomo amesema kuwa CCM imefanya mambo mazuri katika jamii ikiwa ni pamoja na kujenga shule za msingi na sekondari za kata, ambazo zimekuza kiwango cha elimu nchini ikiwa wapinzani wamekuwa wakibeza mafanikio hayo. Pia amewataka wananchi kutokubali maneno ya uchochezi ambayo yamekuwa yakidhoofisha maendeleo  na juhudi za serikali ...

KADA WA CHADEMA AUAWA NYUMBANI KWAKE.

Kamanga na Matukio | 01:51 | 0 comments
Kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mtaa wa Sogea, Makambini mji mdogo wa Tunduma, Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya ameuawa na mtu au watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jumapili ya Desemba 16 mwaka huu nyumbani kwake. Uchunguzi wa awali unadai kuwa kuma mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Meneck Kisunga, alienda nyumbani kwa marehemu, ambaye ni balozi wa mtaa huo akidai nyumbani kwake kuna ugomvi na mkewe hivyo kumtaka marehemu kwenda kusuluhisha ndipo marehemu alipofungua mlango alishambuliwa mpaka kuuawa. Aidha Afisa  Mtendaji wa mtaa huo Bwana Osea Kabula amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na baadae alimtaarifu Mwenyekiti wa Mtaa huo Bwana Ally Mwafongo na hatimae...

MLINZI AUAWA KIKATILI WILAYANI MBOZI MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 01:37 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga, Mbozi.  Simon Mwambene(45) Mkazi wa Kijiji cha Matula, Mbozi Mission Kata ya Magamba Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya, ameuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi alipokuwa lindo. Marehemu ambaye alikuwa ni mlinzi wa binafsi na alikuwa analiza maduka 9 yaliyopo kijijini hapo na aliuawa na watu hao Desemba 13 mwaka huu majira ya saa 8:15 usiku. Maduka hayo yaliyokuwa yakilindwa na marehemu yalikuwa yanamilikiwa na Bwqana Frank Tenson, Mgala, Tweve, Sosten Kibona, Raphael Kisunga, Kamika Simbeye, Crispin Ndabila, Gody Mahenge, Anthon Mwazembe na Samwel Ndabila. Marehemu Mwambene alianza kulinda maduka hayo kwa mkataba kuanzia Desemba 3 mwaka 2011 ambapo hadi...

BREAKING NEWS:- WATU WATATU WAGONGWA NA GARI MKOANI MBEYA MUDA HUU ......

Kamanga na Matukio | 12:31 | 0 comments
 Ajali mbaya imetokea eneo la ILEMI Jijini MBEYA muda huu ambapo gari aina ya TOYOTA LANDCRUISER iliokuwa ikitokea Wilaya ya Chunya imegonga watu watatu huyu ni mmoja wa waliogongwa.  SAMAHANI KWA PICHA HII CHINI NIMELAZIMIKA KUIWEKA ILI UPATE HALI HALISI YA KILICHOTOKEA.  Mwenyezi Mungu ambariki ili aweze kupona. Gari aina ya TOYOTA LANDCRUISER iliokuwa ikitokea Wilaya ya Chunya imegonga watu watatu huyu...

BREAKING NEWS:- MTOTO AUMWA NA NYUKI HADI KUPOTEZA MAISHA.

Kamanga na Matukio | 02:46 | 0 comments
Mtoto wa miaka mitatu na nusu Abiud Moses Mwanyingili mkazi  wa kijiji cha Mponela wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kung'atwa na nyuki alipokuwa akicheza na wenzie kijijini hapo Desemba 13 mwaka huu majira ya saa nane mchana. Katika tukio hilo kundi la nyuki halikuweza kufahamika limetokea wapi, mbali ya kusabaisha kifo hicho pia nyuki hao wamesababisha kifo kwa Ester Kasebele miaka 6 ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi mkoani hapa. Aidha Mwenyekiti wa kijiji cha Mponela Bwana Laniwelo Mwampashi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mazishi ya mtoto huyo yamefanyika kijijini hapo baada ya kufanyiwa uchunguzi na Daktari wa hospitali ya...

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYAHABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 14/12/2012.

Kamanga na Matukio | 02:33 | 0 comments
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE /* Style Definitions */ table.MsoNormalTable {mso-style-name:"Table Normal"; mso-tstyle-rowband-size:0; ...

HABARI KAMILI KUHUSU UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA SONGWE MBEYA WAANZA KUTUMIKA NDEGE ZAIDI YA TATU ZATUA

Kamanga na Matukio | 02:31 | 0 comments
Mwandishi wa habari kutoka Kituo cha redio kinachofahamika kutoka Nyanda za Juu Kusini Bomba FM na Blogu ya Kamanga na Matukio Ndg. Ezekiel Kamanga akishuka katika ndege katika uzinduzi wa uwanja huo wa Ndege wa kimataifa uliopo Songwe Mkoani Mbeya.  Brandy Nelson,Mbeya HATIMAYE  Ndege ya  kwanza ya abiria  imetua  katika Uwanja wa kimataifa wa Songwe rasmi leo baada ya miaka 11 ujenzi wake ambao ...
Pages (14)1234567 Next
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger