Pages


Shirika la viwango Tanzania TBS limepiga marufuku biashara ya uuzwaji wa nguo za ndani za mitumba zinazoingizwa kwenye soko la hapa nchini.

Kamanga na Matukio | 03:58 | 0 comments
Shirika la viwango Tanzania TBS limepiga marufuku biashara ya uuzwaji wa nguo za ndani za mitumba zinazoingizwa kwenye soko la hapa nchini.

Msemaji wa shirika la viwango TBS Bi. Rhoida Andusamile amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa matakwa ya agizo la sheria ya 2009 inayozuia matumizi ya nguo za ndani zilizokwisha tumika.

 Lakini licha ya unafuu wa gharama za upatikanaji wa nguo za mitumba Nchini, Serikali kupitia TBS imepiga marufuku biashara ya uuzwaji wa nguo hizo ikiwemo soksi na nguo za kulalia zoezi linalohusisha Nchi nzima.

Mara nyingi nguo za ndani za mitumba zimekuwa zikitumiwa na jinsia zote mbili lakini wanawake ndiyo wameonekana kuwa wateja wakubwa wa nguo hizo wao walikuwa na maoni gani juu ya kupigwa marufuku uuzwaji wa ngao hizo?.

Kwa upande wao wauzaji wa nguo hizo walikuwa na maneno ya kuongea "Hii ni mara ya pili kwa Shirika la viwango Tanzania - TBS kupiga marufuku biashara ya uuzwaji wa nguo za ndani za mitumba, lakini bado biashara hiyo imekuwa ikishamiri kwa kasi".

 #source-Star Tv#

Hali si Shwari Ndani ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU).

Kamanga na Matukio | 03:57 | 0 comments

 
 Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye akifungua mkutano kati ya waandishi wa Habari na Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)

Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)  wakifuatilia kwa umakini kikao  hicho wakati kikiendelea

  Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye pamoja na katibu wake wakisikiliza kwa umakini wahadhiri wakichangia hoja
  Mmoja wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) , akikazia jambo  ya yale ambayo yalikuwa yamezungumzwa
 Mmoja wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU), akitila  mkazo na kujibu swali ambalo liliulizwa na mmoja wa waandishi wa Habari.
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) wakipiga piga Meza kuashiria kuunga MKONO Hoja ilizo somwa.
 Kikao kikiwa kinafungwa kwa Sala
 Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)  wakiwa wanaimba wimbo wa Solidarity 

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Daniel Mosses Akiwa anauficha Uso akihofia kupigwa picha na kuhojiwa na waandishi wa Habari kuhusiana na Mgogoro unao endelea  Chuoni hapo 

***************

HALI si Shwari  Ndani ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) baada ya Uongozi wa Chama cha Wahadhili wa Chuo hicho (TEKUASA) na wanachama wake kutangaza mgomo wa kutotunga mitihani ya kufungia Mhula, Mitihani ambayo inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu kwa kile walichodai Menejimenti ya Chuo kutotoa majibu ya matatizo yao.
Mgomo huo  umetangazwa leo na Kaimu Mwenyekiti wa Tekuasa Amani Simbeye katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Chuo hicho kilichopo  Block T kata ya Iyela Jiji na Mkoa wa Mbeya na kuhudhuriwa na zaidi ya Wahadhili 30.
Simbeye amesema kuna mambo mengi na changamoto za elimu inayotolewa Chuoni hapo ambazo Menejimenti ya Chuo inahusika moja kwa moja hivyo kuhatarisha mustakabali wa Elimu Nchini hususani inayotolewa Chuoni hapo ambapo ameongeza kuwa zaidi ya yote ni kukosa ushirikishwaji wa maamuzi yanayohusu Taaluma.
Kwa taarifa zaidi na madai ya Wahadhili hao hadi kupelekea kususia kutunga mitihani ya kumaliza muhula inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu yameandikwa kwenye  barua hapo chini lakini habari kamili itawajia baadaye kwa Lugha ya Kiswahili endelea kuwa nasi.








 PICHA , HABARI NA MBEYA YETU

::::: TUZO ZA SOKA ZILIZOTOLEWA NA SPUTANZA :::::;

Kamanga na Matukio | 03:54 | 0 comments
AMRI KIEMBA
Chama cha wachezaji wa soka nchini SPUTANZA kwa udhamini wa Peps mwishoni mwa juma lililopita kilifanikisha azma ya utoaji wa tuzo kwa wachezaji pamoja na makocha waliofanya vyema katika msimu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2012-13.

Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, ilishuhudia wadau wachache wakijitokeza, hali ambayo imepokelewa tofauti na uongozi wa SPUTANZA kwa kukiri japo ni mwanzo wameona walifanya makosa katika utaratibu wa kuitangaza siku hiyo.

Katibu mkuu wa SPUTANZA Said George amesema watayafanyia kazi mapungufu hao kwa kiasi kikubwa ili hafla ya utoaji wa tuzo kwa wachezaji na makocha watakaofanya vizuri msimu ujao iweze kufana.

Katika hafla hiyo inayojulikana kama SPUTANZA FOOTBALL AWARDS wachezaji watatu pamoja na kocha mmoja walizawadiwa baada ya kujizolea kura nyingi zilizopigwa na jopo la makocha.
Tujikumbushie namna ambavyo washindi walivyo tangazwa
1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu - Amri Kiemba (Simba)
Amewashinda
Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu (Yanga),
Kipre Tchetche (Azam),Paul Nonga (Jkt Oljoro)

2. Kocha Bora wa Mwaka - Mecky Maxime (Mtibwa Sugar)
Amewashinda
Boniface Mkwasa (Ruvu shooting),Abdallah Kibaden (Kagera Sugar) Jumanne Charles (Prisons)

3. Mchezaji Bora Chipukizi - Salum Abubakar "Sure Boy" (Azam)
Amewashinda
Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Issa Rashid (Mtibwa)
Shomari Kapombe (Simba) Twaha Shekue (Coastal Union)

4. Golikipa Bora - Hussein Sharif "Casilas" (Mtibwa Sugar)
Amewashinda
Juma Kaseja (Simba), Mwadin Ally (Azam).

Zawadi ya mchezaji bora wa msimu uliopita imekwenda kwa ya kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa Taifa Stars pamoja na klabu ya Simba Amri Kiemba.

Hata hivyo cha kushangaza tuzo ya mchezaji huyo ilipokelewa na mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu ay Dar es salaam Young Africans Mohammed Binda ambae akatoa siri ya kumuwasilisha Amri kiemba.

MMOJA AUWAWA KUFUATIA VURUGU YA WANANCHI WA KIJIJI CHA LUMBILA WILAYA YA MBOZI KUWASHAMBULIA ASKARI WALIOKUWA WANAFANYA OPERESHENI.

Kamanga na Matukio | 01:50 | 0 comments

MKUU WA WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA DR. MICHAEL KADEGE AAKIWATULIZA HASIRA WANAKIJIJI HICHO KABLA YA KUANZA KUWASIKILIZA
                                          DIWANI ATHUMANI   - ACP
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
MKUU WA WILAYA MBOZI BAADA YA KUWATULIZA WANANCHI HAO SASA WANAELEKEA ENEO LA MKUTANO
MOJA YA WANAKIJIJI HICHO AKIELEZEA JINSI TUKIO HILO LA VURUGU LILIVYOTOKEA
AIDHA KATIKA TUKIO HILIO CHARLES   JOSE  MWAWALO,MIAKA 27,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIJERUHIWA KWA KUPATA MICHUBUKO TUMBONI AMBAPO UCHUNGUZI UNAFANYWA KUBAINI NI KITU GANI KILICHOMJERUHI. 
POLISI WALIFANIKIWA KUCHUKUA MADUMU MACHACHE AMBAYO NI MADUMU MATATU YENYE UJAZO WA LITA 60, MADUMU MAWILI YENYE UJAZO WA LITA 20 NA MADUMU NANE LITA 30 HIVYO UVAMIZI HUO WA WANANCHI NDIO ULIOWAFANYA ASKARI POLISI WASHINDWE KUCHUKUA VIELELEZO VYOTE. 



MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUMBILA KATA YA RUANDA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. RAJABU S/O WILSON MWASHITETE, MIAKA 25, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI WALIOKUWA KATIKA MSAKO DHIDI YA WAHALIFU/WAPORAJI KATIKA ENEO LA MLIMA SENJELE.

CHANZO NI BAADA YA ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA OPERESHENI ENEO HILO KUZINGIRWA NA KUNDI LA WANANCHI ZAIDI YA 150 WA KIJIJI HICHO WAKIWA NA SILAHA ZA JADI MAPANGA, MARUNGU, SHOKA NA MAWE WAKIWAZUIA ASKARI HAO KUKAMATA WAHALIFU NA KUANZA KUFANYA VURUGU BAADA YA KUWA WAMEKAMATA MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI AMBAYO NI MAFUTA  AINA YA DIESEL MADUMU ZAIDI YA 100.

HATA HIVYO KUFUATANA NA VURUGU ZILIZOJITOKEZA WALIFANIKIWA KUCHUKUA MADUMU MACHACHE AMBAYO NI MADUMU MATATU YENYE UJAZO WA LITA 60, MADUMU MAWILI YENYE UJAZO WA LITA 20 NA MADUMU NANE LITA 30 HIVYO UVAMIZI HUO WA WANANCHI NDIO ULIOWAFANYA ASKARI POLISI WASHINDWE KUCHUKUA VIELELEZO VYOTE. 

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. 

AIDHA KATIKA TUKIO HILI CHARLES  S/O JOSE  MWAWALO,MIAKA 27,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIJERUHIWA KWA KUPATA MICHUBUKO TUMBONI AMBAPO UCHUNGUZI UNAFANYWA KUBAINI NI KITU GANI KILICHOMJERUHI. 

PIA WANANCHI WALIFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA KWA KUWEKA MAWE NA MAGOGO NA KUSABABISHA MSONGAMANO MKUBWA WA MAGARI BARABARANI. 

HALI ILIKUWA SHWARI BAADA YA KAMANDA WA POLISI KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI PAMOJA NA VIONGOZI WA ENEO HILO KISHA KUFUNGUA BARABARA . 

ASKARI POLISI WANNE WALIJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO KATI YAO WATATU WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA NA ASKARI MMOJA  AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU ZAIDI . 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA BADALA YAKE KUWA NA UTAMADUNI WA KUTATUA KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO KWA KUYAWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA. AIDHA ANAWATAARIFU WALE WOTE WALIOWAHI KUIBIWA/KUPORWA MALI MBALIMBALI YAKIWEMO MAFUTA WAJITOKEZE POLISI KWA AJILI YA HATUA ZINAZOSTAHILI.


Signed By,
                                                            [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Picha na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu

MSHIKEMSHIKE wa Jina la Mkoa Mpya utakaogawanywa kutoka Mkoa wa Mbeya umezidi kushika kasi.

Kamanga na Matukio | 02:32 | 0 comments
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi Ambakisye Minga Alisema hali ya miundombinu ni nzuri katika kila Wilaya zilizopendekezwa na kwamba Wilaya ya Chunya  igawanywe kufuata majimbo ya Uchaguzi kwa Jimbo la Lupa liwe Mkoa wa Mbeya na Songwe kuwa mkoa wa Songwe.


Mkuu huyo wa Wilaya Dk. Kadeghe alitumia Fursa kupiga marufuku uuzaji na ununuaji wa kahawa mbichi maarufu kwa jina la Cherry Wilayani humo kutokana na kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara kuanza kuwarubuni wakulima.


Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo, Elisey Ngoyi alitoa taarifa hiyo huku akitaja Wilaya zitakazounda Mkoa Mpya kuwa ni Mbozi, Momba, Ileje, Chunya, Mbalizi na Igamba ambazo zote zinapitiwa na Mto Songwe.












MSHIKEMSHIKE wa Jina la Mkoa Mpya utakaogawanywa kutoka Mkoa wa Mbeya umezidi kushika kasi baada ya kila pande kupendekeza majina kutokana na maeneo wanayotoka.

Sakata hilo limetokea hivi karibuni baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Momba wakitaka Mkoa huo kuitwa jina la Momba huku Wilaya ya Mbozi ikipendekeza Mkoa Mpya uitwe Songwe.

Wakizungumza katika Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo walisema sababu ya kuitwa kwa Songwe kunatokana na Mto Songwe kupitia Wilaya zote ambazo zitaunda Mkoa Mpya.

Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo, Elisey Ngoyi alitoa taarifa hiyo huku akitaja Wilaya zitakazounda Mkoa Mpya kuwa ni Mbozi, Momba, Ileje, Chunya, Mbalizi na Igamba ambazo zote zinapitiwa na Mto Songwe.

Pia alipendekeza Makao makuu ya Mkoa huo kuwa Tarafa ya Vwawa Wilayani Mbozi kwa kile alichodai kuwa ni katikati ya Wilaya Zote hali itakayowarahisishia wananchi kutembea kwa muda mfupi kutoka Kila Wilaya.

Kauli hiyo pia iliungwa mkono na Baraza zima la Madiwani chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ambakisye Minga walisema hali ya miundombinu ni nzuri katika kila Wilaya zilizopendekezwa na kwamba Wilaya ya Chunya  igawanywe kufuata majimbo ya Uchaguzi kwa Jimbo la Lupa liwe Mkoa wa Mbeya na Songwe kuwa mkoa wa Songwe.

Waliongeza kuwa katika Wilaya hizo zinashabihiana katika mambo mengi yakiwemo Shughuli za kiuchumi , utamaduni , uoto wa asili, ukubwa Kijografia na mazao ya kilimo ambayo hulimwa na kustawi katika Wilaya kama vile Kahawa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Mbozi, Charles Mkombachepa aliwashukuru madiwani kwa michango yao na kwamba Mchakato huo utapelekwa katika Baraza la Ushauri la Wilaya kwa ajili ya kujadiliwa na kupelekwa baraza la Mkoa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Dk. Michael Kadeghe aliwataka wajumbe watakaohudhuria Baraza la Ushauri kusimamia maamuzi yaliyopendekezwa na madiwani yasije yakabadilishwa na kuwakosesha raha wananchi kwa mawazo yao kupitia wawakilishi wao ambao ni madiwani.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Wilaya Dk. Kadeghe alitumia Fursa kupiga marufuku uuzaji na ununuaji wa kahawa mbichi maarufu kwa jina la Cherry Wilayani humo kutokana na kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara kuanza kuwarubuni wakulima.

Alisema wakulima hao hurubuniwa kwa kuuza kahawa hiyo kwa bei ya chini hali ambayo inadidimiza uchumi na kwamba hali hiyo hataivumilia katika Wilaya yake na kuongeza kuwa kwa atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Picha na E. Kamanga

REDD'S MISS MBEYA APATIKANA

Kamanga na Matukio | 02:31 | 0 comments








HATIMAYE  Mkoa wa Mbeya umepata mwakilishi wa kushiriki kinyang’anyiro cha  Mrimbwende wa Redds Miss Tanzania baada ya shindano la kumpata  Miss Mbeya kukamilika Juni 8 mwaka huu.

Mratibu na Mwandaaji Miss Redds Mkoa wa Mbeya kutoka Bomba Entertainment Gabriel Mbwile amesem jumla ya warembo 12 wameshiriki kinynganyiro hicho tangia wawekewe kambi hadi  siku ya shindano.

Ameongea kuwa mshindi wa kwanza amezawadiwa kitita cha fedha taslimu Milioni moja, mshindi  wa pili 750,000/=, mshindi wa tatu 500,000/= na wengine wote wamepewa  kifuta jasho cha  shilingi 100,000/=.

Amewataja washindi hao kuwa ni Jackline Luvanda mshindi wa kwanza, Aneth Brayton mshindi wa pili na Daina  Athlimani aliyeibuka msindi wa tatu.

Amewatja washiriki wengine kuwa ni Naba Magambo, Zainabu Matabi, Salma Abdalah, Flaviana Sixbert, Sarah Samwel, Aisha Beneka, Darlin Athani, Mwajabu Ngobai na Neema Raymond.

Aidha Mgeni rasmi katika kinyang’anyiro hicho  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya  Diwani Athumani, amezidi kusisitiza suala la amani kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya kwamba inapaswa kushughulikiwa ni kila mtu.

PICHA NA MBEYA YETU

Bajeti; Bia, Sigara, Vinywaji Vikali Bei Juu,

Kamanga na Matukio | 02:30 | 0 comments
Photo: Bajeti; Bia, Sigara, Vinywaji Vikali Bei Juu







Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa.
Dar es Salaam, Tanzania. Serikali imeoongeza kodi kwenye magari makuukuu, bia, vinywaji vikali, na baridi ambavyo kodi imekuwa ikiongezwa kila mwaka na kuwathiri watumiaji.


Kutokana na hali hiyo wanywaji pombe na sigara watalazimika kutumia fedha nyingi ili kupata huduma hizo.


Bidhaa zisizokuwa za mafuta ambazo zimefanyiwa marekebisho na kuongezwa kodi ni mvinyo, pombe, vinywaji vikali, na sigara. Vinywaji hivyo vimeongezwa kodi kwa asilimia 10. 


Kutokana na bajeti ya mwaka 2013/14 iliyosomwa jana bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa, Vinywaji vikali vimepanda kutoka Sh2,392 hadi Sh2,631 kwa lita sawa na ongezeko la Sh239 kwa lita moja.


Bia inayotengenezwa kwa nafaka nchini ambayo haijaoteshwa imeongezwa kodi kutoka Sh310 kwa lita hadi Sh341 kwa lita, sawa na ongezeko la Sh31 kwa lita.


Pia bia nyingine zote zimepanda kutoka Sh525 kwa lita hadi Sh578 kwa lita sawa na ongezeko la Sh51 kwa lita.


Kwa upande wa vinywaji baridi, vimeda kutoka Sh83 kwa lita hadi Sh91 kwa lita sawa na Sh na ongezeko la Sh8 kwa lita.


Vile vile sigara zenye kichungi na zinazozalishwa nchini zimepanda kwa asilimia 75, kutoka Sh19,410 hadi Sh21, 351 kwa sigara 1,000 sawa na ongezeko la Sh1.94 na senti 94 kwa sigara moja.




Ushuru pia umeongezwa kwenye magari yasiokuwa ya uzalishaji na yenye umri wa miaka 10 kutoka asilimia 20 mpaka hadi asilimia 25.


Dk Mgimwa alisema hatua hiyo imelenga kupunguza uagizaji wa magari chakavu ili kulinda mazingira na kupunguza ajali za mara kwa mara.


Uamuzi wa serikali kuongeza kodi katika maeneo hayo na mengine, utaisaidia serikali kuongeza mapato ya Sh510 bilioni.

Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa.
Dar es Salaam, Tanzania. Serikali imeoongeza kodi kwenye magari makuukuu, bia, vinywaji vikali, na baridi ambavyo kodi imekuwa ikiongezwa kila mwaka na kuwathiri watumiaji.


Kutokana na hali hiyo wanywaji pombe na sigara watalazimika kutumia fedha nyingi ili kupata huduma hizo.


Bidhaa zisizokuwa za mafuta ambazo zimefanyiwa marekebisho na kuongezwa kodi ni mvinyo, pombe, vinywaji vikali, na sigara. Vinywaji hivyo vimeongezwa kodi kwa asilimia 10. 


Kutokana na bajeti ya mwaka 2013/14 iliyosomwa jana bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa, Vinywaji vikali vimepanda kutoka Sh2,392 hadi Sh2,631 kwa lita sawa na ongezeko la Sh239 kwa lita moja.


Bia inayotengenezwa kwa nafaka nchini ambayo haijaoteshwa imeongezwa kodi kutoka Sh310 kwa lita hadi Sh341 kwa lita, sawa na ongezeko la Sh31 kwa lita.


Pia bia nyingine zote zimepanda kutoka Sh525 kwa lita hadi Sh578 kwa lita sawa na ongezeko la Sh51 kwa lita.


Kwa upande wa vinywaji baridi, vimeda kutoka Sh83 kwa lita hadi Sh91 kwa lita sawa na Sh na ongezeko la Sh8 kwa lita.


Vile vile sigara zenye kichungi na zinazozalishwa nchini zimepanda kwa asilimia 75, kutoka Sh19,410 hadi Sh21, 351 kwa sigara 1,000 sawa na ongezeko la Sh1.94 na senti 94 kwa sigara moja.





Ushuru pia umeongezwa kwenye magari yasiokuwa ya uzalishaji na yenye umri wa miaka 10 kutoka asilimia 20 mpaka hadi asilimia 25.


Dk Mgimwa alisema hatua hiyo imelenga kupunguza uagizaji wa magari chakavu ili kulinda mazingira na kupunguza ajali za mara kwa mara.


Uamuzi wa serikali kuongeza kodi katika maeneo hayo na mengine, utaisaidia serikali kuongeza mapato ya Sh510 bilioni.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger