Pages


AJINYONGA KWA KUTUMIA MKANDA WA SURUALI YAKE KATIKA OFISI YA KIJIJI.

Kamanga na Matukio | 05:16 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
*Ni baada ya kukamatwa na Uongozi wa Kijiji.
*Chanzo ni Mishikaki ya Shilingi 1,000/=
Mkazi wa Kitongoji cha Gezaulole, Kijiji cha Haporoto Kata ya Ihango Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya Mbwiga Mwandele(50 -55)  amejinyonga kwa kutumia mkanda wa Suruali yake katika Ofisi ya kijiji hicho.

Tukio hilo limetokea Oktoba 26 mwaka huu majira ya saa mbili usiku na maiti yake kugunduliwa Oktoba 27 saa mbili asubuhi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa marehemu kabla hajafikwa na mauti alidaiwa deni la shilingi 1000 ambayo inadaiwa kuwa alikula mishikaki(nyama) eneo la Kilabu cha Kijiji cha Haporoto, ambapo huuza pombe za kienyeji na marehemu kushindwa kulipia mishikaki na kupelekwa katika Ofisi ya kijiji.

Aidha Uongozi wa Kijiji hicho chini ya Mwenyekiti wake Bwana Daimon Mndewa alimwachia jukumu mgambo wa kijiji hicho Bwana Fredy Wiston, kumlinda marehemu ili asubuhi ya Oktoba 27 suala hilo lizungumzwe lakini ilipofika asubuhi mgambo huyo alikuta Mwiga amejinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali aliokuwa ameuvaa marehemu kabla ya kifo chake.

Kwa upande wake  Mke wa marehemu Bi Malita Mbwiga(45) amesema waliachana na mumewe muda mfupi walipokuwa wakinywa pombe na yeye kuamua kurejea nyumbani na marehemu hakurejea nyumbani na baadae alipata taarifa ya kuwa kajinyonga katika Ofisi ya kijiji Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa mbili asubuhi.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Gezaulole Bwna Raphael Jailos Mbenya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na mwili wa marehemu ulichukuliwa na jeshi la polisi hadi hospitali ya Rufaa jijini Mbeya na kwamba Jeshi la polisi linawashikilia Mwenyekiti wa kijiji na mgambo kwa mahojiano na kwamba wakati wa tukio Afisa Mtendaji wa kijiji Bwana Mwalingo Mbenya hakuwepo kijijini hapo.

MGANGA WA JADI AUAWA BAADA YA WATEJA WAKE KUTOPATA MATOKEO MAZURI YA MATATIZO YAO.

Kamanga na Matukio | 05:14 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga,Mbeya Vijijini.
*Wamlipa Mganga shilingi 600,000/=
*Waacha ujumbe wanakijiji wasihusishwe.
Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamemuua kwa kumkatakata na mapanga kisha kumpiga nyundo utosini Mganga wa Jadi, aliyetambuliwa kwa jina l.a Mlenga Mwazowa(60 - 65, mkazi wa Kitongoji cha Izumbwe, Kijiji cha Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya.

Tukio hilo limetokea Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa sita usiku, ambapo watu hao walivunja nyumba ya mganga huyo kisha kumtoa nje na kuanza kumchalanga kwa mapanga na kisha kumpiga nyundo ya utosini, ambapo alifariki papo hapo mita chache kutoka kwenye nyumba yake.

Imedaiwa kuwa mganga huyo alikuwa na ahadi na wateja wake ambao walilipa kiasi cha shilingi 600,000 kwa minajili ya kutimiziwa malengo yao lakini baada ya kulipa kiasi hicho na kutofikiwa wanaji hao walimfuata na kumtaka arudishe pesa hizo lakini Mganga huyo alishindwa ndipo walipotekeleza azma yao kisha kuacha ujumbe kwenye karatasi ulioandikwa "ASIKAMATWE MTU YEYOTE KATIKA TUKIO HILI KWANI MGANGA AMEKULA LAKI SITA ZETU NA HAJATEKELEZA AHADI YETU" ulimaliza ujumbe huo na kwamba tumetoka Ngolongo.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana Herman Mwanyinaga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba aliamshwa majira ya saa saba usiku na alifika eneo la tukio na kwamba wakati ukatili huo unafanyika mke wa marehemu alikuwa ndani na wanawe watatu.

Mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu zake baada ya kufanyiwa uchunguzi na Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Inyula kilichopo wilayani humo.

Hata hivyo hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hili na mazishi yalifanyika nyumbani kwa marehemu Oktoba 27 majira ya saa saba mchana. 

MTOTO WA MIAKA 8 AJINYONGA KWA KUTUMIA KAMBA YA VIATU.

Kamanga na Matukio | 05:14 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Iwambi, darasa la tatu Kervin Patrick (8) jinsi ya kiume amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu katika bomba ya maji nje ya nyumba yao.

Tukio hilo limetokea Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa 5 kamili usiku wakati wazazi wote wa mtoto huyo Bwna Patrick Mwakapalila(52) na Bi Subira Patrick(30) wakiwa hawapo nyumbani na kwamba baba mzazi akiwa na mwanae wa kiume aitwaye Joshua Patrick(10) waliondoka majira ya saa 3:30 kuelekea mjini.

Aidha Baba wa mtoto huyo alipigiwa simu na mtu mmoja kwamba arejee nyumbani na yeye pasipo kuchelewa alirejea na kumkuta mwanae amejinyonga katika bomba la maji kwa kutumia kamba ya viatu na chini kukiwa na ndoo, ambapo kifo hicho kimezua maswali mengi kwani kimo cha mtoto ni zaidi ya futi mbili na nusu na urefu wa kamba hali inayotia shaka kuwa mtoto huyo alichukua uamuzi huo yeye mwenyewe.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Ivwanga Bwna Chonde Kalisto amethibitisha tukio hilo la kusikitisha na kwamba yeye alipokea taarifa kutoka kwa Balozi wake Bi Esther Mahenge ambapo walitoa taarifa polisi ambapo walifika eneo la tukio kisha kuuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi na hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.

PICHA TANO ZA TUKIO LA MWANAFUNZI NA MTU MZIMA KUJINYONGA MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:13 | 0 comments
 Mwili wa Mwanafunzi wa darasa la tatu, Shule ya Msingi Iwambi, Jijini Mbeya Kervin Patrick (8) jinsi ya kiume ukiwa umefunikwa baada ya kufariki dunia kutokana na kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu katika bomba ya maji nje ya nyumba yao.
 Baadhi ya majirani waliojitokeza kushuhudia mwili Mwili wa Mwanafunzi wa darasa la tatu, Shule ya Msingi Iwambi, Jijini Mbeya Kervin Patrick (8)
 Mama mzazi wa marehemu Kervin Patrick (8)Bi Subira Patrick(38) akiwa katika hali ya majonzi kufuatika kifo cha mwanae aliyejinyonga.
Baadhi ya mashuhuda wakiwa wamekusanyika kushuhudia Mwili wa Mkazi wa Kitongoji cha Gezaulole, Kijiji cha Haporoto Kata ya Ihango Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya Mbwiga Mwandele(50 -55)  amejinyonga kwa kutumia mkanda wa Suruali yake katika Ofisi ya kijiji hicho.
Mke wa marehemu Mbwiga Bi Malita Mbwiga(45) wa pili kutoka kulia akiwa na baadhi ya akina mama waliofika kumfariji kufuatia kifo cha mumewe(Picha na Ezekiel Kamanga,Mbeya)

MWANDISHI WA HABARI TBC AIBIWA KAMERA NA KOMPYUTA PAKATO(LAPTOP) CHUMBANI KWAKE.

Kamanga na Matukio | 05:20 | 0 comments
Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1)  Ndugu Hosea Cheyo.
 
Habari na Ezekiel Kamanga, Iringa.
Mwandishi wa habari wa wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC1 mkoani Mbeya Bwana Hosea Cheyo ameibiwa Kamera na kompyuta pakato yaani Laptop vyenye thamani ya shilingi 1,800,000 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Happy Lodge iliyopo jirani na kituo kikuu cha mabasi cha Iringa, Oktoba 2 mwaka huu majira ya 1:30 asubuhi.

Mwandishi wa habari huyo alikuwa mkoani Iringa kuhudhuria semina ya waandishi wa habri wa Nyanda za Juu Kusini inayohusu mchakato wa Katiba iliyoandaliwa na Baraza la Habari nchini MCT kuanzia Oktoba 22 mwaka huu hadi Oktoba 24 mwaka huu katika Ukumbi wa Maktaba uliopo Manispaa ya Iringa.

Bwana Cheyo amesema Oktoba 24 asubuhi alipokuwa kuoga alifunga mlango kwa ufunguo na aliporudi alishangaa kuona vifaa vyake havipo, hali iliyomfanya kutoa taarifa kwa mhudumu wa nyumba hito ya kulala wageni na hakuwa na maelezo ya kutosha.

Mwandishi huyo amedai kuwa mbinu iliyotumika kufungua mlango wake ni kutumia ufunguo bandia na kisha wezi hao kuingia kiurahisichumbani humo na kuondoka na vifaa vyake vya kazi.

Aidha Bwana Cheyoaliotoa taarifa Kituo cha Polisi Mkoani humo na kufunguliwa jalada lenye namba IR/RB/6350/012 na kwamba Jeshi la polisi linamshikilia mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni kwa mahojiano zaidi.

Hata hivyo ilibidi Bwana Cheyo kushindwa kuendelea na semina  ili kushughulikia tatizo hilo, huku Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoani Mbeya Bwana Christopher Nyenyembe, amempa pole  mwandishi huyo wa TBC kwa kuibiwa nyaraka muhimu na kuwataka wamiliki wa nyumba za wageni kukomesha vitendo vya wizi vinavyofanywa na wahudumu wao.

AFA KATIKA NYUMBA YA IBADA AKIABUDU NA MWINGINE AJINYONGA BAADA YA KUMPIGA MKEWE.

Kamanga na Matukio | 05:19 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Mary Jimmy (55 - 60), Mkazi wa Barabara ya Tatu, Sokomatola Jijini Mbeya amefariki dunia alipokuwa aliabudu katika Ibada ya asubuhi(Morning Glory) kwenye Kanisa moja kubwa eneo la Kabwe jijini hapa Oktoba 23 mwaka huu.

Tukio hilo lilimetokea majira ya saa 1:30 asubuhi ambapo imedaiwa kuwa marehemu alifika kanisani hapo  majira ya saa 12:30 kwa nia ya kufanya ibada ndipo akiwa katika maombi alianguka chini na waumini walifanya maombi bila mafanikio mpaka walipoamua kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa na kuthibitisha kifo chake.

Mdogo wa marehemu ambaye hakupenda kutajwa jina lake kwa madai kuwa si msemaji wa familia alisema kuwa marehemu aliondoka nyumbani akiwa mzima kabisa hivyo kifo hicho kimemshitua mno.

Mwili wa marehemu unafanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Rufaa na mazishi yanataraji kufanyika leo katika makaburi ya Nonde jijini hapa. Marehemu ameacha mtoto mmoja wa kiume.

Tukio jingine Mkazi mmoja wa Iziwa, Jijini hapa Mbwiga Mwalungwe(60), amefariki dunia baada ya kujinyonga nyumbani kwake kwa kutumia waya wa simu Oktoba 24 mwaka huu baada ya marehemu kumpiga mkewe.

Inadaiwa marehemu alimpiga mkewe aitwaye Bi. Taines Mbwiga(45) Oktoba 23 hali iliyompelekea kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini hapa ambapo alipewa PF3 kwa ajili ya kutibiwa na kulazimu kulazwa hospitalini hapo.

Baada ya mkewe kulazwa hospitalini, Jeshi la Polisi lilianza kufuatilia tukio hilo ndipo marehemu alipogundua kuwa anakabiliwa na mkono wa sheria aliamua kuchukua uamuzi mgumu kwa kuchukua waya wa simu majira ya saa 4 kamili asubuhi Oktoba 24, kisha kujinyonga nyumbani kwake.

Aidha polisi walifika eneo la tukio majira ya saa 6:00 mchana na kuuchukua mwili wa marehemu hadi hospitali ya rufaa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hata hivyo hali ya Bi, Taines inaendelea vema ambapo ameruhusiwa kutoka hospitalini Oktoba 2 na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali hiyo.

Kwa upande wake Balozi wa mtaa huo Bwana Chaina Juma amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba anawaachia jeshi la polisi kufanya uchunguzi ili kupata kiini hasa cha Bwana Mwalungwe kujiua kwa kujinyonga.

WATU 14 WAFUTIWA MASHTAKA YA KOSA LA JINAI.

Kamanga na Matukio | 05:18 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbozi.
Bwana Paulo Sichone na wenzake 13 wote Wakazi wa Kijiji cha Myunga, Kata ya Myunga, Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya wamefutiwa mashtaka  wamejikuta wakibubujikwa na machozi ya furaha baada ya kuachiwa huru na mahakama ya wilaya ya Mbozi mkoani hapo Oktoba 2 mwaka huu.

 Watu hao walikuwa wakikabiliwa na kesi namba 143/2012, wakituhumiwa kwa kosa la kutumia silaha na unyang'anyi ambapo kwa pamoja wanadaiwa kuvunja nyumba ya Bwana Benard Simundwe na kuiba mali zenye thamani ya shilingi milioni 87, kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 287(a).

"Kwa pamoja mheshimiwa naiomba mahakama yako Tukufu kuwaachia huru washtakiwa wote, kwa kutumia Kifungu cha 91 cha sheria na Jamhuri haina nia ya kuendelea na kesi hiyo" alisema muendesha mashtaka mahakamani hapo.

Baada ya kauli hiyo ya mwendesha mashtaka, Wakili wa washtakiwa mheshimiwa Edgar Bantulaki alikubaliana na mwendesha mashtaka, hivyo wateja wake kuwa huru kuanzia Oktoba 25 mwaka huu tangu walipokamatwa Agosti 13 mwaka huu na wengi wao kudhalilishwa na Jeshi la Polisi wakati wa operatioh hiyo.

Aidha baada ya kesi hiyo kumalizika mahakamani washtakiwa hao walilakiwa na ndugu zao wakiongezwa na Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Satiel Japhet Sikanyika na Diwani wa kata ya Iyunga Bwana mheshimiwa Godfrey Siame ambao kwa pamoja wamesema wanamshukuru Mungu kwa shari lao kumalizika kwani shughuli za uchumi zilizorota kijijini hapo kwani muda mwingi walikuwa wakiutumia kuhudhuria kesi ya mahakamani na gharama kubwa za nauli kutoka Myumba.

Kwa upande wake nje ya mahakama wakili Edgar aliwataka wananchi hao kutokuwa na risasi hivyo wasamehe na kupotezea kabisa hivyo wasamehe na kusahau yote yaliyopita.

Pia Mcungaji wa Kanisa la Moravian Tanazania, Jimbo la kusini Magharibi, Mchungaji Isaya Simsokwe amewaambia wananchi wa Kijiji cha Myunga kumtegemea Mungu wakati wao ndio maana ametetea na kuwashindia katika kesi hiyo nzito ambayo imesababisha wengine kuuza Chakula ili kukabiliana na keshi hiyo.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mlalamikaji katika kesi hiyo Bwana Benard Simunde, alionekana mahakamani hapo hali inayotia shaka utendaji wa Jeshi la Polisi kwa kufadhili mtandao wa uhalifu, licha ya kukabiliwa na kuhusika na vitendo vya mauaji lakini Polisi wamekuwa wakimwangalia bila kuchukua hatua zozote na wakati meingine kunywa nae juice kama ilivyokuwa imetokea Oktoba 25  Bwana Simundwe alipokuwa  na askai katika mgahawa uliopo Posta eneo la Kiwila Mbozi.

Hata hivyo vielelezp vilivyowasilishwa kituo cha Tunduma na Mbozi vimetoweka katika hali ya Tunduma na Mbozi vimetoweka katika hali ya kutatanisha ilinayompa wakati mgumu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athumani vilivyodhibiti vitendo vya rushwa vilivyokithiri katika vituo mbalimbali .

AJALI:- MSIKILIZE KEPTENI WA TIMU YA TANZANIA PRISONS AKIZUNGUMZIA AJALI WALIYOIPATA.

Kamanga na Matukio | 04:17 | 0 comments
Na Greyson Chris Bee Salufu/Chimbuko Letu.
Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Soka ya Tanzania Prisons inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ya Mkoani Mbeya wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka mara tatu ambapo watu watano wamejeruhiwa, majira ya saa 5 usiku wa kuamkia leo wakati wakielekea Mkoani Tanga kwa ajili ya mechi dhidi ya Mgambo JKT itakayofanyika siku ya Jumamosi Oktoba 27 mwaka huu mkoani hapo.

Akizungumza kupitikia Kipindi cha Bomba Special Show cha Bomba FM redio 104.0MHz kinachorusha matangazo yake kutoka Mkoani Mbeya, Nyanda za Juu  Kusini Kepteni wa Timu hiyo Shaban, amesema gari hilo lilikuwa na jumla ya watu 30 na chanzo cha ajali hiyo imetoakana na gari kubwa la mizigo lililokuwa likija mbele yao kwa mwendokasi na wakati dereva wao alipojaribu kulikwepa gari hilo la mizigo ndipo lilipopinduka mara tatu.

Ameongeza kuwa wachezaji wanne na kiongozi wao mkuu wa msafara ndio waliokimbizwa Hospitalini usiku huu kutokana na hali zao kuwa tete na Jeshi la Polisi lilifika mapema katika tukio hilo.

Sikiliza hapa Kepteni wa timu hiyo akizungumza moja kwa moja kupitikia Kipindi cha Bomba Special Show cha Bomba FM redio 104.0MHz:-

TEOFILIO KISANJI UNIVERSITY CONVOCATION ON 2ND NOVEMBER 2012

Kamanga na Matukio | 04:37 | 0 comments

The Convocation Executive Committee of The University of Teofilio Kisanji (TEKU) requests the attendance of all TEKU Convocation Members to the annual Convocation on 2nd November 2012 at the TEKU Hall, on the main campus of TEKU University in Mbeya, at 9.30 am.


This year the Convocation will proudly host Dr. Johnson Ishengoma of The University of Dar-Es-Salaam, as keynote speaker. Dr. Johnson Ishengoma will address the Convocation on the theme of The Challenges of Financing Higher Education in Tanzania –with special attention to the problems and issues of private Universities in Tanzania.


Dr. Johnson Ishengoma is a Senior Lecturer and the Head of Department, Educational Foundations, Management and Lifelong Learning, School of Education at University of Dar-Es-Salaam and he has written and researched extensively on the questions of education and higher learning finance. Some of his research interests are: Higher Education in Africa, Higher Education Financing and Quality Assurance and Control in Education. His published work includes: Ishengoma, Johnson M (2007a) Access and Equity in Higher Education: Assessing Financing Policies-A Comparative Study of Seven African Countries. Tanzania Report, Report submitted to the Sizanang Research and Development Center, Pretoria, South Africa; PhD Dissertation:  “Cost Sharing and Participation in Higher Education in Sub-Saharan Africa:  The Case of Tanzania.”; Ishengoma,  Johnson, PhD Dissertation:  “Cost Sharing and Participation in Higher Education in Sub-Saharan Africa:  The Case of Tanzania.” Some of his articles available on the web and online are Ishengoma, Johnson M (November 24 2011) “North-South Partnerships Are Not the Answer,”  http://www.scidev.nt/en/science-and-innovation-policy/opinions/north-south-partnerships-are-not-the-answer-1.html# (Science and Development Network); Ishengoma, Johnson M (2003) (First Quarter) “The Myths and Realities of Higher Education Globalization: A View from the Southern Hemisphere,” http://www.escotet.org/infocus/forum/ishengoma.htm Ishengoma, Johnson M (2002a) “Financing Higher Education in Post-Apartheid South Africa: Trends, Developments and Challenges Ahead,” http://www.gse.buffalo.edu/org/IntHigherEdFinance ; Ishengoma, Johnson M (2002b) “Towards the Termination of Foreign Aid in Sub Saharan Africa: A Proposal and Reflections from an African Perspective,” http://www.fiuc.org/iaup/esap.  



All senior management and permanent academic staff, members of The University Council, all graduates and diplomates and graduate, diploma and certificate course students and those awarded honorary degrees by Teofilio Kisanji University and retired academic employees are most welcome to attend this Convocation. Your attendance and participation will be highly appreciated. 


Mpeli Nsekela

President

Teofilio Kisanji University Convocation

MAKALA YA MBEGU FEKI

Kamanga na Matukio | 02:32 | 0 comments
Na Esther Macha,
SERIKALI ya Tanzania ilitangaza sera ya Kilimo Kwanza kama njia maalumu ya kitaifa ya kuongeza kasi ya kuleta mapinduzi ya kilimo nchini na kuinua pato la wakulima Kwanza inajumuisha mikakati inayolenga katika kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili kilimo chetu na kutumia fursa lukuki tulizonazo kujiondolea umaskini wa kipato.

Azima ya Kilimo Kwanza ilibuniwa chini ya Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) ambalo ni mfumo wa mashauriano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye mwenyekiti wa Baraza hilo.

Licha ya nchi yetu kuwa na hekta milioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo, ni asilimia 23 tu ndiyo inayotumika. Kuna hekta milioni 29 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na maji ya kutosha yapo lakini ni asilimia moja tu iliyo chini ya umwagiliaji.

Aidha, licha ya Tanzania kuwa na maziwa na mito yenye maji ya eneo la kilomita za mraba 62,000, ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi wenye urefu wa kilomita 1,424 na kilomita za mraba 223,000 za ukanda maalumu wa kiuchumi baharini (Exclusive Economic Zone), lakini maji hayo mchango wake kwa pato la taifa na la mtu mmoja mmoja bado ni hafifu .

Kilimo kinachangia asilimia 95 ya chakula kinachotumika nchini, asilimia 30 ya mauzo nje na asilimia 65 ya malighafi zinazotumika katika viwanda vyetu vya ndani.

Kujitosheleza kwa chakula ni muhimu kwa usalama na utulivu wa nchi yetu, pia itasaidia kupunguza mfumuko wa bei kwani chakula huchangia kiasi cha asilimia 55.9 katika kupima kiwango cha mfumuko wa bei.

Kilimo ni kiungo muhimu cha sekta mbalimbali katika kuchangia kutimiza malengo ya kukuza uchumi wa taifa. Ni dhahiri kwamba hatuwezi kufuta umaskini bila kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo. Kwa jumla ili Tanzania iweze kufikia malengo yake ya maendeleo sekta ya kilimo inatakiwa ikue kutoka asilimia nne hivi sasa na kufikia angalau asilimia 10.

Kwa kutambua umuhimu wa kilimo katika nchi yetu, kwa nyakati mbalimbali, zimefanyika jitihada maalumu za kuendeleza kilimo.

Mafanikio ya kilimo kwa kiasi fulani yamepatikana lakini bado hakijapata nafasi ya kumwondolea Mtanzania umaskini wa kipato, bado yuko taabani kimaisha.

Kutokana na umuhimu wa kilimo katika maendeleo yetu, ilitakiwa kipewe kipaumbele mkubwa ili kuinua maisha ya watu ambayo yanategeme kilimo cha mvua, ambayo si ya uhakika.

Hivyo, ni wajibu wa serikali na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo kuhakikisha kwamba sera ya Kilimo Kwanza inamkwamua kiuhalisia mkulima, hasa mdogo, kwa kumuwezesha kulima kisasa.

Kwa kuzingatia hilo hivi karibuni mwandishi wa makala alitembelea katika kijiji cha Ichesa Kata ya Myovisi ,Wilaya ya Mbozi Mkoani  Mbeya kufuatilia malamiko ya wakulima  kuumwa matumbo baada ya kula ugali unaodaiwa kutokana na mbegu feki ya  mahindi ya njano inayodaiwa kusambazwa na wakala mmoja kijijini hapo.

Akizungumza na gazeti hili mmoja wa wakulima hao Bi.Joliga Ndwina anasema kutokana na adha hiyo wakulima hao wameziomba mamlaka husika na watafiti kulifuatilia kwa kina suala la ununuzi wa vocha za mbolea ya ruzuku kutoka kwa wakulima kumuuzia wakala kwa bei ya kati ya sh.2,000 hadi Sh.4,000 unaodaiwa kufanywa na wakala mmoja jina limehifadhiwa.

“Sawa tunaweza kulaumu wakala kwa haraka lakini mtu ambaye anatakiwa kulaumiwa hapa ni Kampuni ya PANNAR kwani wao ndo walimpa wakala wao kusambaza mbegu hizo,mahindi haya hayana soko kabisa pili  matumbo yanauma sana tukila ugali wake tunaomba serikali itusaidie katika hili  hali mbaya kwakweli nah ii kampuni ichungwe kuhusu mbegu hizi haiwezekani sisi tuumie wakati wengine wanapata raha”anasema mama huyo.

 “Hili suala ni la muda mrefu sana hapa kijijini lakini wataalamu mbali mbali wamekuwa wakifika lakini hatuna huyu wakala kuchukuliwa hatua zozote zaidi ya kuona tu mtaalamu huyu anakuja na Yule lakini kinachofanyika”anasema.

Wakizungumza na  gazeti hili baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ichesa (majina tunayo)walisema kuna hatari kubwa kwa mwaka huu waananchi wa Kijiji hicho kukumbwa na baa LA njaa na hali ya uchumi

kushuka kutokana na kusambaziwa mbegu inayotoa unga wa njano inayodaiwa ya kampuni ya pannar na hivyo kukosa kabisa soko.

Bw.Nasibu Mwashilindi anasema kuwa  wamejitahidi kwenda kuuza mahindi hayo kwa sh. debe sh.2,000 katika soko la mazao Mlowo licha ya bei ya mahindi kwa debe kupanda hadi kufikia sh.6,000 lakini hayanunuliwi na kurudi nayo majumbani.

"Hali ni mbaya ndugu zangu haya mahindi ni shida kwani hakuna anayenunua kutokana na ugali wake kuwa mchungu mdomoni na hata upande wa soko bado ni tatizo sana sisi wananchi wa kijiji cha Ichesa tuna
wakati mgumu sana kwani uchumu wetu wa maisha ni mgumu kufuatia hali hii kwani hatujui haya mahindi tutayapeleka wapi mpaka sasa"anasema mwananchi huyo.

Bw.Mwashilindi anasema kibaya zaidi mahindi hayo hayaliki kutokana na uchungu wa ugali wake hasa ukipoa na wengine wanalalamika watoto wao kuumwa matumbo wanapokula jambo ambalo wamehofia kuwa linaweza kuleta athari kiafya.

Hata hivyo baadhi ya wakulima hao wamesema  kuwa mbegu hizo zilizokuwa rangi ya njano wameuziwa na wakala huyo ambapo mfuko umeonesha zimetoka katika kampuni ya Pannar lakini katika jambo la kushangaza hata kibunzi ni chekundu na imefikia hatua wananyanyapaliwa katika mashine za kusaga
kama watu wenye kimela cha kutengenezea pombe.

"Tunapokwenda kusaga mashine wanatuambia tusubiri hadi wamalize kusaga wenye mahindi meupe na sisi ndiyo tunakuwa wa mwisho hata kama tumewahi,sababu ni kwamba nikitangulia mimi mwenye mahindi ya njano na wote watakaofuatia hata wakiwa na mahindi meupe yanabadilika kuwa
njano,"walisema.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ichesa,Bw.Paul Mwasenga anasema walipokea vocha za ruzuku za pembejeo 600 za mbolea aina ya Urea ya kukuzia mwezi februari,2012 na kwamba kweli vocha za mbolea ya kupandia aina ya CAN hazikufika kabisa.

Aidha Bw.Mwasenga alikanusha kusikia taarifa ya wakala kununua vocha za ruzuku kwa Sh.2,000 amekanusha vikali na kudai hizo ni njama za kuchafuana kisiasa na hakuna kitu kama hicho ingawa alifafanua.

Mtendaji huyo amekiri kupata malalamiko ya kuwepo mbegu feki ya mahindi ambayo imekuja kubainika baada ya mahindi kukomaa na kwamba wakulima walinunua mbegu hiyo katika maeneo tofauti ikiwemo kwa wakala Ntandala wa Kijiji cha Ichesa ambaye ndiye alikuwa akisambaza Kata ya
Myovisi.
Mjumbe wa kamati ya ugawaji wa vocha ya Kijiji cha Ichesa,Bw.Mashaka Mwashambwa anasema  hajawahi kusikia madai hayo na kazi wanayoifanya kamati ni kubwa kwani kabla ya kugawa wanatoa elimu kuhusu thamani ya vocha na punguzo lililotolewa na serikali baada ya kuitisha mkutano wa
hadhara na baadaye walitembelea mashamba na kugawa vocha kwa wahusika.

Hata hivyo wajumbe wengine watano kati ya sita akiwemo Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Vocha ya kijiji cha Ichesa hawakuweza kupatikana kuelezea sakata hilo.

Ofisa kilimo Kata ya Myovisi Bw.Danfod  Mandali   amethibitisha kupokea malalamiko ya mbegu feki  na hivyo alichukuwa hatua ya kuwasiliana na Ofisa wa kilimo Wilaya ya Mbozi ambaye alifika na timu
ya wataalamu waliwahoji wakulima na kuchukua sample.

Bw.Mandali anasema  suala la madai ya baadhji ya wakulima kuuza vocha kwa wakala halijamfikia rasm,i ila kuna tetesi mitaani wakulima wakiwataja wenzao wanaolalamika kuuza kwa bei ya chini vocha hizo baada ya kuziona hazina kazi tena kutokana na mazao yao kukomaa.

"Wakulima ni kama asilimia 40 walioathirika na mbegu hiyo na kuhusu kuuza vocha  nimewahi kuwasikia wakulima wakiwataja wenzao waliouza kwa wakala huyo  lakini wanaficha ficha kuhofia kukosa kupata katika msimu unaokuja  kwa sababu kisheria ni makosa...huku ilikuja UREA tena kwa kuchelewa mwezi Machi,mbegu na mbolea ya kupandia walisema imehifadhiwa mkoani watapewa mwezi septemba, kwa ajili ya msimu wa 2012 na 2013,"alisema.

Wakala aliyedaiwa kugawa mbegu na kununua vocha katika kijiji cha Ichesa, Bw.Japhet Ntandala alipohojiwa kuhusiana na tuhuma hizo alikanusha na kulaani vikali kwamba wanataka kumchafua mbele ya wananchi wake na kwamba yupo tayari kununua mahindi yote kwa wale aliowauzia mbegu ili wananchi wake wasife na njaa.

Wakala huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kijiji hicho anasema  hajawahi kununua vocha na angependa mtu aliyedai amemuuzia ajitokeze ili azungumze ukweli na yupo tayari kufika naye mahakamani ili sheria iweze kuchukuwa mkondo wake.

Ofisa Kilimo Mkoa wa Mbeya ,Dkt.Philipo Mwaisoba alishukuru kupata taarifa hiyo na kuahidi kufuatilia huku akidai ni hatari kubwa endapo vocha za ruzuku zimeuzwa tena kwa wakala kwani ni makosa  sheria na kwamba atafuatilia kujuwa mbegu hizo zinazodaiwa feki na kutolea majibu.

Hata hivyo Gazeti hili lilimtafuta Mwakilishi wa Kampuni ya Pannar  inayodaiwa kusambaza mbegu hizo feki Bw.Tulio  ambaye baada kuulizwa na gazeti hili alisema kuwa   hakuna mbegu feki katika kampuni yake na kusema kuwa watafika katika kijiji hicho kuangalia ni nani aliyesambaza mbegu hizo.

“Hawa najua ni watu au makampuni yanayotupiga vita kuhusiana na utoaji wa mbegu  zetu ,sisi mbegu zetu ni bora.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa kuna taarifa ya kusambazwa kwa mbegu hizo feki karibu maeneo mengi ya Wilaya ya Mbozi na kuna hofu ya wananchi walio wengi kupata madhara ya kiafya na hali ngumu ya maisha kutokana na mahindi hayo kukataliwa na wanunuzi wa mazao.

RC MBEYA AWAONYA WANAOANZISHA VYUO VYA UFUNDI STADI KIENYEJI

Kamanga na Matukio | 02:29 | 0 comments
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh Abbas Kandoro.
 Na Esther Macha, Mbeya
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro ameonya tabia ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakianzisha vyuo  vya Ufundi Stadi kienyeji bila ya kuwa na usajili wowote kutoka serikalini hali ambayo imekuwa ikirudisha nyuma  maendeleo ya elimu ya ufundi nchini.

Amesema kuwa vyuo vingi vya ufundi vimekuwa vikianzishwa tu bila kufuata utaratibu wowote na wahusika na hivyo kusababisha wanafunzi kukosa sifa za kufanya mtihani yao ya mwisho.

Bw. Kandoro aliyasema hayo jana wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wamiliki wa Vyuo vya ufundi stadi,pamoja na wakuu wa  vyuo vya ufundi stadi na secretariat ya Veta Kanda ambapo mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa mikutao wa veta uliopo chuoni hapo.

“Hali hii inasikitisha sana ukitembea mitaani huko vyuo vimejazana lakini havina usajili na kwamba hali hiyo inapoteza muda sana kwa vijana wetu  kwani baadaye huambiwa hawana namba za usajili wakati wa kufanya ,mitihani yao ya mwisho kutokana na kutokuwa na namba za usajili ambazo zinasababisha vyuo hivyo kuendeshwa bila kufuata utaratibu na sheria”alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Hata hivyo alisema kuwa kama mkoa hawana tatizo na watu ambao wanaanzisha vyuo kwani lengo lao ni zuri la kuhakikisha kuwa kila kijana anapata ajira badala ya kukaa vijiweni,kikubwa  ni kufuata taratibu za serikali ili kuwa na usajili halali.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema vyuo vikiwa vingi vitasaidia vijana kuwa na elimu ambayo ni endelevu na kwamba kupitia ufundi huo vijana wanazpata ujuzi wa ufrundi mbali mbali.

Aidha Bw. Kandoro aliwashauri wazazi na vijana  kuona kuwa elimu ya ufundi  stadi ni mchepuo mwingine wa elimu na sio chaguo la mwisho mara wanapokosa  fursa  ya kuendelea  na elimu ya sekondari  au elimu ya juu.

Alisema wazazi wana wajibu kuweka kipaumbele elimu ya ufundi kwani ni sawa na elimu nyingine ambazo zimekuwa zikipewa nafasi .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Veta Kanda ya Kusini Magharibi Bw.Justine Rutta alisema maqfunzo hayo yatajumuisha washiriki kutoka mikoa ya , Mbeya, Rukwa pamoja na Kata na kwamba mkutano huo utakuwa na washiriki 64 ambao utakuwa na wamiliki  wa vyuo vya ufundi stadi,wadau mbali mbali wa elimu   na mafunzo ya ufundi ,wakuu wa vyuo vya ufundi stadi.

Bw. Rutta alisema kuwa katikia mafunzo hayo kila chuo kitasoma taarifa fupi ya chuo chake ili kufahamu mapungufu yaliyopo ,pamoja na  miongozo na taratibu za usajili wa vyuo ili kuwa na vyuo vya ufundi stadi vyenye hadhi  bora.

MAKUNDI YALIYOGAWANYIKA NDANI YA CCM NI CHANZO CHA KUPOTEZA VITI VYA UBUNGE

Kamanga na Matukio | 02:26 | 0 comments
Na Ester Macha,
NAIBU waziri wa  Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw.Adam Malima amesema kuwa sababu kubwa ambayo inayochangia kupoteza viti vya ubunge katika maeneo mbalimbali nchini ni kutokana na makundi yaliyogawanyika ndani ya chama kipindi cha kura za maoni ndani ya chama hicho.

Amesema kuwa makosa ambayo huwa yanafanyika wakati wa kupitisha majina ambapo jina linalopitishwa linakuwa sio chaguo la wanachama  hivyo hulazimika kumpa mtu yeyote kutokana na chama kuweka jina ambalo halitakiwi kwa wanachama.

Bw. Malima alisema yote inatokana  na chama cha mapinduzi kupoteza viti vya ubunge katika maeneo mbali mbali ni kutokana wagombea walio wengi kukataliwa kwenye kura za maoni ndani ya chama hicho.

Akitolea mfano Mkoa wa Iringa alisema kwamba Mbunge wa sasa Mchungaji Msigwa hana uwezo wa kuwa Mbunge katika jimbo la Iringa bali wananchi walilazimika kumchagua kutokana na kura za maoni  ndani ya ccm katika kumchakato wa kumchagua mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo..

Bw. Malima alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama cha mapinduzi uliofanyika katika viwanja vya sokoine Jijini hapa.
 
“Mfano tosha tunao kutoka Mkoa wa Iringa jina lililopitishwa ndani ya halmashauri kuu ya CCM  halikuwa chaguo la wanachama  hivyo wananchi wote wakalazimika kumchagua Mbunge ambaye hakupaswa kuwa mbunge “alisema Bw. malima.

Akizungumzia kwa Mkoa wa Mbeya alisema kuwa kwamba kwa kawaida Mbeya ni ya chama cha mapinduzi lakini katika uchaguzi uliopita walijikwaa ndio maana ilifika mahala wakapoteza viti viwili  vya ubunge ambavyo ni Mbeya Mjini na Mbozi Magharibi.

Alisema kuwa hata Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bw.Mbilinyi nae hana uwezo wa kuingia bungeni na kuwatetea wananchi wake hali kadhalika na Mbozi magharibi pia hawafanani na wananchi wanaowaongoza ambao wanatakiwa kwenda kuwatetea bungeni bali yote hiyo ilitokana na kujikwaa kwa chama .

Hata hivyo alisema kwamba katika chaguzi mbali mbali ndani ya chama cha mapinduzi ni sawa na usajili wa timu ambayo itakayokwenda kushindana mwaka 2015 hivyo makosa yaliyofanyika kipindi kilichopita inatakiwa kuyarekebisha sasa  ili kuondokana na makundi yasiyokuwa na tija ndani ya chama cha mapinduzi ambayo yamekuwa yakitoa nafasi ya kushinda kwa vyama vya upinzani .

“Uchaguzi huu ambao tunafanya leo ni usajili wa timu itakayokwenda kushindana kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 hivyo ni vema tukawa na timu nzuri ambayo itakuwa na nguvu kubwa na upinzani kushindwa kutumia mianya hiyo ambayo imekuwa ikitoa nafasi  kubwa kwa wapinzani kupenye kwa kutumia makundi yetu ndani ya chama”alisema Malima.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger