Pages


WA 3 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 03:48 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Jeshi  la polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu watatu kwa kosa la kuingia nchini bila kibali katika kijiji cha Isyonje wilaya ya Rungwe mkoani hapa..
.
Kamanda wa Polisi Advocate Nyombi amesema tukio hilo limetokea majira ya saa moja asubuhi Februari 28 wakiongozwa na  Ahil Ally (26) akiwa na wenzake wawili katika msafara huo.

Aidha Kamanda Nyombi ameongeza kuwa mbinu iliyotumika ni kwa njia ya kificho ambapo walikamatwa na polisi waliokuwa doria na watuhumiwa wapo mahabusu wakati upelelezi juu ya tukio hilo unaendelea.

MCHUNGAJI AJIMILIKISHA ENEO LA MTU NA KUFANYIA IBADA.

Kamanga na Matukio | 03:46 | 0 comments

 Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mchungaji Elia Jongo wa kanisa la Church Of God  la Air port jijini Mbeya baada ya eneo la alilokuwa ameazimwa kwa muda kwa  ajili ya kuendeshea ibada na kudai kuwa eneo hilo kuwa ni lake.

Mchungaji Jongo alivamia eneo hilo linalomilikiwa na Bwana Allen Mwakyoma mwaka 2007 na kupiga hema ambalo alikuwa akiendeshea ibada bila kumwomba mmiliki wa eneo hilo ambalo aliliuza kwa Anyingisye Msokwa  ambaye naye hakuwa ameliendeleza na hivyo mchungaji huyo kuendelea kufanyia ibada zake.

Sakata hilo liliingia sura mpya baada ya Februari 22 katika siku ya jumapili Anyingisye Msokwa  kumwaga mawe katika eneo hilo na ambapo alimwambia mchungaji Jongo atafute eneo jingine lakini badala yake mchungaji alienda mahakamani Februari 23 na mahakama kuwataka Anita Mwakyoma  na Anyingisye msouwa kupewa pingamizi na mahakama kutaka wasiliendeze eneo hilo.

Hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa mchungaji hana nyaraka zozote zinazohusiana na eneo hilo licha ya kudai kuwa ni eneo lake na lina thamani ya sahilingi milioni arobaini kauli ambayo ilipingwa na bwana Allen Mwakyoma ambaye pia alipinga mkewe kuingizwa katika suala ambalo halimuhusu.

Hata hivyo Jeshi la polisi limelazimiaka kuingilia kati kwa kumtuma askari wake Pc Mbwana baada ya kupigiwa simu  na mchungaji Jongo kwamba amevamiwa naye alipofika  katika eneo hilo alikuta hali ndivyo sivyo na kudai hawezi kumkamata mtu yeyote bila kupata hati ya mahakama.
      

ANYWA SUMU NA KUPOTEZA UHAI BAADA YA KUPOTEZA SHILINGI ELFU KUMI NA TATU - MBEYA

Kamanga na Matukio | 03:44 | 0 comments
Habari na mwandishi wetu.
Shida Sasumba (37) mkazi wa Sinde jijini Mbeya amekunywa sumu na kumsababishia mauti baada ya kupoteza shilingi elfu kumi na tatu.

Kwa mujibu wa mashuhuda ambao hawakupenda majina yao kutajwa wamesema wakati wanapitisha michango kwa wakazi wa mtaa huo kwa ajili ya kusafirisha mwili wa marehemu Shida kuelekea katika wilaya ya Kyela mkoni Mbeya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana Jakobu Mwalyepere amesema kuwa marehemu alikunywa sumu Februari 26 mwaka huu, na badaye alichukuliwa na kupelekwa katika Kituo cha polisi cha Kati kilichopo jijini hapa ambapo alipewa PF3 na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini Mbeya.

Aidha Mwalyepele aliongeza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa mkoni Mbeya kwa ajili ya kusubilia taratibu za kusafilisha mwili huo kuelekea katika wilaya ya kyela mkoni hapa.

Pia taaRIfa zinaeleza kuwa marehemu alikuwa na mtoto mmoja ambaye anajulikana kwa jina la Hawa Sasumba ambaye alikuwa akiishi naye katika mtaa huo.

 Hata Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya  Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hosipitali ya Rufaa mkoani hapa.

SHULE YA SEKONDARI YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WANAFUNZI KUTOKANA NA IDADI YA VYUMBA VYA MADARASA- MBOZI

Kamanga na Matukio | 03:42 | 0 comments
Habari na Angelica Sullusi, Mbeya.
Shule ya Sekondari ya Kata ya Msangano Wilayani Mbozi inakabiliwa na upungufu wa wanafunzi kulingana na idadi ya vyumba vya madarasa vilivyopo shuleni hapo.

Akizungumza ofisini, Mratibu Elimu wa Kata hiyo  Osiah Mwanyamba amesema kuwa upungufu huo unatokana na ufaulu mdogo uliopo katani hapo kwa wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi.

Mwanyamba ametaja sababu inayofanya kuwepo na ufaulu mdogo katika shule za msingi katani hapo kuwa ni uhaba wa walimu katika shule hizo za msingi zipatazo tano,unaotokana na ugumu wa mazingira ya kufundishia kwa mwalimu lakini pia kujifunzia kwa mwanafunzi.

Ameongeza kuwa sababu nyingine ni uelewa mdogo wa wakazi wa maeneo hayo kwani bado wanakumbatia mila za zamani kwamba mtoto wa kike ni wa kuolewa tu,na hata wakiume hulazimika kwenda mashambani kulima hasa nyakati za msimu wa kilimo.

Aidha,Mwanyamba ameishauri serikali kutupia macho kata hiyo katika suala zima la kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia pamoja na kutoa elimu kwa wananchi wa maeneo hayo ili kuboresha elimu katani hapo.

WAZEE WA KIMILA WAMEKEMEA VITENDO VYA KIOVU MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 03:14 | 0 comments
Wazee wa kimila mkoani Mbeya kwa kushirikiana na Kikundi cha Polisi jamii ulinzi shirikishi wamendelea kupinga na kukemea  vitendo vya upigaji nondo, mauji ya watoto wasio kuwa na hatia na wizi wa mali za watu unaofanywa na baadhi ya watu.

Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa  chama cha MJATA mkoani hapa Bwana  Shayo Soja Makoko alipokuwa akihutubia katika mkutano uliofanyikia katika kijiji cha Nsanga Mwelu Mbeya vijijini ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na machifu kutoka  wilaya mbalimbali  zilizopo mkoni hapa wakishirikiana na  kikundi cha polisi jamii.

Chifu Makoko alisema kuwa chama hicho kipo kwa ajili ya kupambana na maovu yote yanayojitokeza katika ndani ya jamii ili kuhakikisha matatizo yanayojitokeza katika jamii zetu kuhakikisha yanaondolewa mara moja.

Aidha Makoko aliongeza kuwa chama cha MJATA kilianzishwa na mchifu kwa lengo la kusaidiana na serikali kwa lengo la kupambana na kukomesha vitendo vya kiovu ndani ya jamii.

Naye mjumbe kutoka katika kikundi cha polisi jamii mkoani hapa Bwana Pita Mwakasembwa  aliwataka wananchi pamoja na machifu kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi badala yake washirikiane na Jeshi la polisi katika kutoa taarifa zinazojitokeza katika jamii pindi wahalifu wanapowakamata.(Kwa habari zaidi soma hapa Chimbuko Letu Blog)

AGONGWA NA GARI LA MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 03:14 | 0 comments
Habari na Mwandishi wetu.
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Shamwengo Wilaya ya Mbeya vijijini Mkoani Mbeya aligongwa na moja ya mgari yaliyokuwa kwenye msafara wa Ziara ya siku tatu ya Makamu wa Rais Dakta Mohammed Gharib Bilal mkoani hapa.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi na mbili jioni  Februari 25 mwaka huu wakati msafara wa magari wa kutokea Wilaya ya Mbarali kuelekea Jijini Mbeya.

Majeruhi alifahamika kwa jina la Franu Elia (28) ambapo aligongwa na gari hilo wakati akiendesha baiskeri  wakati msafara huo ulipokuwa unapita.

Pia Franu  aliokotwa na msamalia mwema Faines Mwalemba , Agnes  Kahawa  ambao waliomba msaada katika gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T 247  BFL lililokuwa likiendeshwa na Bwana John Mgaya  na msaidizi wake Justin Milaji ambao walimpeleka katika kituo cha polisi  cha  Inyala  na kupewa PF3 na kisha kuelekea Kituo cha afya  cha Inyala.
 
Hata hivyo kutokana na kujeruhiwa vibaya sehemu ya kichwani hali iliyopelekea kuvuja damu nyingi, wauguzi wa kituo cha afya Inyala walimtaka mgonjwa kupelekwe hospitali ya RUFAA jijini Mbeya, ambapo amelazwa mpaka sasa.

Lakini jitihada za kumtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Advocate Nyombi ali aweze kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo  ziligonga mwamba kutokana na Kamanda huyo kuwa katika msafara huo.

WATU 2 WAFARIKI DUNIA KATIKA MATUKIO 2 TOFAUTI MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 03:13 | 0 comments
Habari na Mwanishi wetu
Watu wawili wamefariki dunia katika matukio  mawili tofauti mkoani Mbeya yaliyotokea Februari 26 mwaka huu.

Katika tukio la kwanza lilitokea majira ya saa nane mchana katika eneo la Nzovwe katika barabara ya Mbeya/Tunduma ambapo Hamisi Fusa (35), mkazi wa Simike aligongwa na gari lisilofahamika .

Chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi  na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa jijini Mbeya na huku Jeshi la polisi likifanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

Na katika tukio jingine ambalo lilitokea Tunduma katika wilaya ya Mbozi mkoani hapa mtu mmoja asiyefahamika jina lake (20) aliuwawa na watu wasiofahamika baada ya kukatwa katwa na vifaa vyenye ncha kali kisha mwili wake kutupwa katika moja ya madarasa ya shule ya msingi Tunduma.

Na chanzo cha mauaji bado hakijafahamika na Polisi bado wanafanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

Adha katika majira ya saa tano asubuhi mwendesha pikipiki asiyefahamika katika eneo la Chimala katika barabara ya MBEA/IRINGA aliingilia kati msafara wa Makamu wa Rais alipokuwa anaelekea mkoani Iringa na kusababisha moja ya magari kupinduka .

Gari lenye namba za usajili  STU 2429, ambapo ndani ya gari hilo lililopinduka alikuwemo Mbunge wa Viti maalum wa mkoa wa  Mbeya (CCM)  Hilda Ngoye, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Beatha Swai  pamoja na dereva wa gari hilo  wamekimbizwa katika hosipitali ya Rufaa mkoani Mbeya.

YALIYOJILI KATIKA ZIARA YA MAKAMU WA RAIS DAKTA BILALI KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:37 | 0 comments
 Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal akisamilimiana na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wakati wa ziara yake katika Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Phillip Mulugo akijibu swali la Diwani wa Kata ya Tunduma Bwana Frenk Mwakajoka kuhusiana na zoezi la uandikishwaji wa watoto wa darasa ya la kwamba ambapo Waziri Mulugo amesema kuanzia siku ya Jumatatu Februari 26 watoto wote wanaostahili kwenda shule waanze masomo mara moja na ifikapo mwezi Aprili atakuja kukagua kama wanafunzi hao wamekwishaanza masomo..
 Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal akifungua lango la Soko la Tunduma lililoungua mwishoni mwa mwaka uliopita wakati wa ziara yake katika Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
 Baadhi ya halaiki ya wananchi wa Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi waliohudhuria katika ufunguzi wa Soko la Tunduma lililoungua mwishoni mwa mwaka uliopita.
 Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal akisamilimiana na mlemavu mwenye shati la blue Bwana Martine Teonas, wakati wa ziara yake katika Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
 Mkuu wa wilaya ya Mbozi Mheshimiwa Gabriel Kimoro wa kwanza kutoka kulia.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mheshimiwa Abbas Kandoro akihutubia wananchi huku akiwasihi wananchi hao kumsikiliza Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal wakati wa ziara yake katika Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
 Mkuu wa Kituo cha Polisi Tunduma A.S. Wendo (kulia) baada ya kutuliza mukali wa vijana wa Mji mdogo wa Tunduma, katika Ziara ya Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal mjini hapo.
 Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia wananchi wa Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, wakati wa ziara yake ya uzinduzi wa vituo vya huduma za jamii, kama masoko n.k.
Mbunge wa Jimbo la Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde ambaye naye akiwaasa wananchi kuwa watulivu ili kumsikiliza Makamu wa Rais na kusahau yaliyotokea, ambaye anakuja kwa shughuli za Kiserikali na sio kisiasa na kama kuna tatizo lolote basi ni muda muafaka wa kumuuliza Makamu wa Rais ili kutafutiwa ufumbuzi.
 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi, akipongezana na Diwani wa Kata ya Tunduma Frenk Mwakajoka baada ya kurejesha amani na utulivu wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Bilal
 Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Phillip Mulugo (kulia), akipokea maelezo kutoka kwa Afisa Elimu mkoa Bwana Juma Kaponda (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki mheshimiwa Godfrey Zambi (katikati) wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Bilal
 Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal akisamilimiana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbozi, wakati wa ziara yake katika Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
 Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na wananchi wakati akiwasili katika Viwanja vya soko la Tunduma, wakati wa ziara yake katika Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
 Diwani wa Kata ya Tunduma Frenk Mwakajoka akitoa malalamiko kutokana na tatizo la kutofanyika kwa zoezi la uandikishwaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza.
Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mwenyekiti wa Haki za Binadamu wilaya ya Mpya ya Momba Bwana Stephano Simwaza, wakati wa ziara yake katika Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.(Picha zote na Ezekiel Kamanga,Mbeya)

SILAHA, KETE ZA BANGI NA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI, WATU SABA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 02:12 | 0 comments
Habari na Mwandishi wetu.
Jeshi la polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kuingia nchiini bila kibali, kukutwa na kete za bangi na kumiliki silaha ambapo ni kinyume cha sheria.

Akizungumzia kutokea kwa matukio hayo Kaimu  Kamanda wa Polisi mkoani hapa Barakiel Masaki  amesema kuwa katika tukio la kwanza lilitokea Februari 23, mwaka huu maeneo ya Uyole  jijini Mbeya, ambapo Polisi wakiwa doria walimkamata Bwana Fakaso Ugala (25) raia wa Ethiopia pamoja na wenzake watatu  kwa  kosa la kuingia nchini bila kibali.

Katika tukio jingine  lililotokea siku hiyo hiyo majira ya saa kumi jioni katika eneo ya Mlowo katika wilaya ya Mbozi mkoani hapa  Bwana Ezila Chilenga Mlamba (31) ambaye ni mfanyabiashara alikamatwa akiwa na bangi kete 815 ambazo ni sawa na kilo 1 na gramu 125 akiwa ameficha katika kibanda chake cha biashara.

Hata hivyo tukio la mwisho lilitokea majira ya saba mchana katika kijiji cha Ipande katika wilaya ya Kyela Atambwile Mwakalukwa  (25) na Dankeni Mwakalukwa (40)  wote wakazi wa Kijiji cha Taratara walikamatwa na silaha aina ya short gun lemingi ston yenye namba NN 505220 V na risasi 30.

Aidha Masaki ameongeza kuwa watuhumiwa wote wapo mahabusu  na upelelezi unaendelea juu ya matukio hayo.

MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA MBEYA, MARY MWANJELWA AMETOA MSAADA WA MASHINE YA KUANGUA VIFARANGA VYA KUKU.

Kamanga na Matukio | 02:11 | 0 comments
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Dokta Mary Mwanjelwa akizungumza na wananchi wa soko la sido Mwanjelwa jijini Mbeya, ataka watendaji wabovu kuondolewa ili kuweka heshima kwa serikali.
*****
Habari na Mwandishi wetu
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, Mary Mwanjelwa ametoa msaada wa mashine ya kuangua vifaranga vya kuku yenye thamani ya Shilingi milioni nne kwa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Kyela.

Akikabidhi msaada huo Mbunge huyo amesema maisha ya wanawake lazima yabadilike kutoka katika hali ya utegemezi na kuanza kuzisaidia familia zao kupitia jitihada zao wenyewe kupitia miradi ya mbalimbali.

Dakta Mwanjelwa amesema ni wakati kwa wanawake kutambua fursa za kimaendeleo zilizopo ikiwemo kujiunga katika Vikundi vya wajasiriamali ili kuwarahisishia wadau kuweza kuwasaidia.

Akipokea msaada huo Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya, Tabu Lugwesa aliwaomba wadau wengine kusaidia jumui za wanawake ili waweze kujikomboa dhidi ya utegemezi na kuwataka wanawake walipatiwa msaada huo kujituma na kuutumia msaada huo kama ulivyokusudiwa.(Kwa hisani ya Chimbuko Letu Blog)

MKUTANO WA UJIRANI MWEMA

Kamanga na Matukio | 02:33 | 0 comments
Kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbozi Bwana Gabriel Kimoro akiwa na Mkuu wa wilaya ya Nakonde nchi ya Zambia Bwana James Singoi  na viongozi wengine wa wilaya hizo katika mkutano wa ujirani mwema uliofanyika katika wilaya ya Mbozi hivi karibuni. Dhumuni la mkutano huo ilikuwa ni kuimarisha ulinzi na usalama mpakani pia kudhibiti uhamiaji haramu. (Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya)

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI BI ROSE MUHANDO AINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA SONY

Kamanga na Matukio | 02:04 | 0 comments



EAST AFRICAN GOSPEL STAR ROSE MUHANDO SIGNS MULTI-RECORD DEAL WITH SONY MUSIC

Global recording company Sony Music Entertainment is proud to announce the signing of East African Gospel Star Rose Muhando to its roster of artists, which includes some of the most important recordings in history. The signing was announced at a press conference in Dares Salaam, Tanzania on the 9th February 2011, and is the first deal of its kind for East Africa.
Rose Muhando is undoubtedly one of Africa’s biggest selling and most acclaimed gospel artists, with millions of fans throughout East Africa and her home country Tanzania. The gospel diva has now been signed to a multi-album recording deal with Sony Music, and a fullservices management deal with Sony Music and ROCKSTAR4000.
Sony Music Entertainment Africa views the continent of Africa as a highly important music development frontier and believes that some of the best talent in theWorld is currently creating and performing music across the continent. Sony has set its sights on becoming the primary partner of the best Africa has to offer and has high hopes that with its assistance, African musicians can achieve new Pan African and Global success.
“We’re so excited about the wealth of talent we are discovering literally daily inAfrica.” says Managing Director of Sony Music Entertainment Africa Sean Watson. “Rose is a magnificent example of the level of talent we mean to invest in. Her gift is quite extraordinary and we are very proud to be her partner. We count her alongside us as a pioneer of a new era in African music.”

 'Its a new and exciting time for amazing talent and music from Africa to shine and we are thrilled to have a star like Rose as part of the family and to represent Rose through the next chapter of her very successful career' said Jandre Louw, CEO of ROCKSTAR4000 Music Entertainment.
 
‘I am thrilled and honored to be working with great African talents. Rose Mhando is a new addition to this roaster of clients that embodies what Rockstar 4000 believes and stands for. She is an Iconic local Tanzanian brand that we will develop to become an International brand’ added Christine Seven Mosha, Music and New business of ROCKSTAR4000

Rose was so excited and thanked God for all he has blessed her with.
Rose Muhando was born in 1976 and was raised in Dodoma, Tanzania. On being deathly ill, Rose converted to Christianity and it was this move, her leading the choir at her local church and her meeting Nassan Wami that prompted her first album recording.
Today Rose lives in Dar Es Salaam where her career has flourished over the last 10 years.  To date, Rose's first album shattered sales records, selling over 5 million copies. She currently has her second album (JipangeSawaSawa) out, which has already sold well over 1.3 million copies.  The magical voice has not been restricted to Tanzania and she has toured extensively across the African continent, covering cities in Kenya, Mozambique, South Africa, Malawi. Congo, Uganda. Rose has also been well received in the United States. 
For more information contact:
Tabasamu Pr Consultancy
+255 754 602674
ROCKSTAR4000 MEDIA & PRESS:
 
Follow us on:

=====================================================================
ABOUT SONY MUSIC ENTERTAINMENT:
=====================================================================

Sony Music Entertainment is a global recorded music company with a current roster that includes a broad array of both local artists and international superstars. The company boasts a vast catalog that comprises some of the most importantrecordings in history. It is home to premier record labels representing music from every genre, including American Recordings, Arista Nashville, Arista Records, Battery Records, Beach Street Records, BNA Records, Columbia Nashville, Columbia Records, Day 1, Epic Records, Essential Records, Flicker Records, J Records, Jive Records, LaFace Records, Legacy Recordings, MASTERWORKS, Polo Grounds, RCA Records, RCA Nashville, RCA Red Seal, RCA Victor, Reunion Records, Roc Nation, Sony Classical, Sony Music Latin, Star Time International, Verity Gospel Music Group, and Volcano Entertainment. Sony Music Entertainment is a wholly owned subsidiary of Sony Corporation of America. 
=====================================================================
ABOUT ROCKSTAR 4000 MUSIC ENTERTAINMENT:
=====================================================================

ROCKSTAR4000 is the first PanAfrican Music Solutions Company, as well as a content, digital and events production network.  It is home to the largest Pan African roster of current artists across the African continent that includes a broad array of Africa’s superstars from the vast spectrum of music genres that influence the African continent’s music trends.
ROCKSTAR4000 Music Entertainment has recently been announced as one of the TOP2 Music Companies worldwide byMIDEM, France. This accolade is for the most innovative and creative use ofmusic with brands in marketing campaigns worldwide
ROCKSTAR4000 provides brands an unrivalled mix & reach of the best entertainment based experiences fromaround the world and across Africa on a local level!  We believe in, develop and drive best-­-of-­-breed teams of skilled individuals across Africa to deliver the best music experiences on par and beyond the best productions in the world – made in Africa!
WELCOME TO THE REST OF YOUR LIFE...!
 
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger