Pages


MFANYABIASHARA MKOANI MBEYA AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA SHIMO LA CHOO,

Kamanga na Matukio | 04:13 | 0 comments
Na mwandishi wetu
Bariki Sanga mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa Uyole jijini Mbeya ambaye alikuwa akifanya biashara ya ulanguzi wa mpunga katika kijiji cha Wimba mahango kata ya Igurusi amekutwa akiwa amefariki dunia ndani ya shimo la Choo huku mwili wake ukiwa umeharibika vibaya.

Mwili wake umekutwa ndani ya choo ukiwa umewekwa kwenye gunia na kufungwa na nguo mbalimbali jana majira ya saa kumi za jioni baada ya ndugu na marafiki kumtafuta kwa zaidi ya wiki moja.

Kutokana na tukio hilo mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Witson Kazimoto amewataka wananchi wa kijiji hicho washirikiane na Jeshi la polisi ili kuweza kumpata Bariki Mbariko ambaye anadaiwa kuwa mara ya mwisho alikuwa na marehemu na walikuwa wamekubaliana kwenda kulangua mpunga.

Inadaiwa kuwa marehemu huyo alikuwa na fedha taslimu shilingi laki sita na alizikwa jana usiku jirani na eneo alilokutwa kutokana na mwili wake kuharibika vibaya hivyo kushindikana kusafirishwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa hadi sasa Jeshi la polisi linawashikiria watu wawili kwa kuhusika na tukio hilo.

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUNASWA NA UMEME MBEYA

Kamanga na Matukio | 03:27 | 0 comments
Na mwandishi wetu
Mtoto Atanasi Aloni mwenye umri wa miaka 13 na mwanafunzi wa shule wa darasa la nne shule ya msingi Msongwi amefariki dunia baada ya kunaswa na umeme akiwa kwenye harakati ya kukata matawi ya miti iliyokuwa jirani na nyaya za umeme.

Tukio hilo limetokea leo hii majira ya saa 3 kamili za asubuhi ambapo mtoto huyo akiwa na kaka yake Ezekiel alifikwa na mauti baada ya tawi alilokuwa analikata kundondokea kwenye umeme wa gridi ya Taifa eneo la Pipe line kata ya Mwakibete jijini hapa.

Habari zaidi zinadai kuwa kabla ya mtoto huyo kufikwa na mauti alikuwa na mama yake mzazi shambani wakipanda mahindi na muda mfupi ndipo kaka yake limwita na kumuomba mdogo wake apande juu ya mti kwa ajili ya kukata matawi kwa mujibu wa mama wa mtoto huyo Bi.Tabu Mwakalenga.

Aidha kuhusu tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema kuwa hajafikishwa taarifa na kuahidi kuzitolea ufafanuzi baada ya kumfikia ofisini kwake.

HALI YA TUNDUMA BAADA YA AJALI YA MOTO NI MAJONZI, RC AWAPA POLE

Kamanga na Matukio | 03:26 | 0 comments
Mkuu wa mkoa wa Mbeya akizungumza na wafanyabiashara wa Tunduma baada ya tukio la ajali ya Moto  jana jioni ambapo amewapa pole kutokana na maafa hayo.
Watu wakiokota mabaki ya vitu vilivyoungua kwenye maduka ya eneo la TUNDUMA maarufu kama Mansese
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro akitembelea eneo ambako moto umetekeza maduka katika mji wa Tunduma
Moto ukiendelea kuwaka kutokana  na ajali iliyotokea jana jioni na kusababisha hasara ya mabilion  ya fedha katika mji wa Tunduma wilayani Mbozi(kwa hisani ya Indaba Africa)

MOTO MKUBWA WATEKETEZA SOKO LA KISIMANI - TUNDUMA - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:51 | 0 comments
Mkuu wa wilaya ya Mbozi Bwana Gilbert Kimolo akipewa maelekezo na mikakati ya kudhibiti moto uliokuwa ukiendelea katika soko la Kisimani mji mdogo wa Tunduma.
*****
Na Ezekiel Kamanga
Moto mkubwa umeteketeza kabisa soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma wilaya mpya ya Momba mkoani Mbeya, jana na kusababisha hasara kubwa ya mali kuteketea na baadhi ya watu kujeruhiwa.

Zaidi ya wafanyabiashara elfu moja wameathiriwa kiuchumi kutokana na moto huo ulioanza majira ya saa 10 jioni mara umeme ulipo rudi baada ya kukatika na hivyo kusababisha moto kuzuka katikati ya vibanda ndani ya soko.

Juhudi za kuuzima moto huo zilichukua muda kutokana na mji huo wa kibiashara kukosa gari la zima moto, hali iliyolazimu magari ya maji(boza) yanayotumika kujenga barabara kutoka Mji wa Tunduma kwenda mkoani Rukwa kusaidia kudhibiti moto huo na kusaidiwa na magari mawili ya zima moto kutoka wilaya ya Nakonde ya nchini Zambia ambapo nayo yalishindwa kuzima moto huo.

Hata hivyo magari mawili kutoka jijini Mbeya yalifika eneo la tukio majira ya saa moja na robo usiku ili kudhibiti moto huo.

Uhaba wa maji katika mji huo umechangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha shughuli za uzimaji moto huo kwani magari kutoka nchini Zambia yaliishiwa maji mapema.

Mkuu wa wilaya ya Mbozi Bwana Gilbert Kimolo alifika mapema kutoa pole kwa wahanga na kuwaomba kuwa watulivu kutokana na janga kubwa lililowakuta na kwamba serikali inafanya uchunguzi ili kuweza kubaini chanzo hicho cha moto.

SOKO LA KISIMANI MJI MDOGO WA TUNDUMA LILIVYOTEKETEA KWA MOTO.

Kamanga na Matukio | 05:34 | 0 comments
Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya limeteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo. Chanzo hakijaweza kubainishwa lakini inadaiwa kuwa Umeme uliporudi baada ya kukatika ndipo moto ulipoanza katikati ya Soko hilo
Vibanda vilivyokuwa vimejengwa kwa mbao vimeteketea na kubakia masalia ya mabati yaliyotumika kuezekea vibanda hivyo katika Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya, jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Kijana mmoja aliyevalia mwenye fulana ya Bluu akiwa amekamatwa wakati akijaribu kutorosha baadhi ya mali zilizokolewa katika moja ya maduka yaliyoteketea kwa moto katika soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya , jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa wamebeba mizigo ya mali zao mara baada ya kufanikiwa kuokoa mali zao katika Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya lililoteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Baadhi ya wafanyabiashara wakipakia mizigo ya mali zao katika gari  mara baada ya kufanikiwa kuokoa mali zao katika Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya lililoteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Askali wa kampuni ya Ulinzi akitizama mali iliyookolewa katika moja ya maduka ambapo wananchi waligombania mali hizo na kuzichukua wakati Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya likiendelea kuteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Mbao zilizokuwa zimetumika kujengea vibanda vya biashara zikiwa zimevunjwa ikiwa ni moja ya njia ya kudhibiti moto kutoendelea kuteketeza vibanda, maduka na mali za wafanyabiashara katika soko la soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya lililoteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Pichani ni duka ni moja wapo ambalo halikuweza kuteketea kwa moto, ambapo ukitazama juu ya paa Paka aliyekuwa na rangi Nyeusi hakuweza kutoweka hapo, licha wa moto kuendelea kuteketeza maduka na vibanda vya biashara katika soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya lililoteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Magari ya kampuni ya Ujenzi wa barabara ya Tunduma mpaka Sumbawanga yalifika kutoa msaada wa kudibiti moto katika Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya lililoteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.  
Gari la zimamoto likiwasili eneo la tukio kudhibiti moto kutoendelea kuteketeza maduka, vibanda vya biashara na bidhaa katika soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya lililoteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
 Mkuu wa wilaya ya Mbozi Bwana Gilbert Kimolo(mwenye suti ya rangi ya kijivu) akiwa katika hekaheka za kutaka kushuhudia soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya lililoteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Mzee huyu alishikwa na bumbuwazi la kutoamini duka lake likiteketea kwa moto ambapo hivi karibuni aliingiza mzingo wa bidhaa kutoka jijini Dar es salaam uliogharimu shilingi milioni Ishirini.

UKATILI DHIDI YA VIKONGWE KWA IMANI ZA KISHRIKINA ULIOKUWA UMESHAMIRI MIKOA YA KASKAZINI SASA VYASHAMIRI MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:57 | 0 comments
Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani), akiwa hoi jana siku ya jumapili baada ya kupingwa na wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya wakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina.
Mkuu wa kituo cha polisi cha Iyunga(kushoto) na Mwenyekiti wa kitongoji cha Ikuti Bwana Emanuel Mwasote(katikati mwenye shati ya pink) wakijaribu kuokoa maisha ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani), kwa kumpeleka Kituo cha polisi Iyunga, baada ya wananchi wenye hasira kali kuvamia kwenye nyumba yake na kutaka kuichoma moto jana siku ya jumapili kabla ya kupingwa na wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya wakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina. Hata hivyo juhudi hizo ziligonga mwamba baada ya wananchi hao kuwazidi nguvu polisi kutokana na  Jeshi la polisi kushindwa kufika mapema eneo la tukio na kuaanza kumdondoshea kichapo.
 Bwana Richard Mwakalinga akijaribu kuokoa maisha ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani),wakati wananchi wa kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga jijini hapa kuanza kumdondoshea kichapo jana siku ya jumapiliwakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina, wakati Jeshi la polisi halijafika eneo la tukio ili kuwedha kuwadhibiti wananchi hao.
Wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya, wakimpiga kwa mawe Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani), hapo jana siku ya jumapili  wakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina.
 Hapa ni nyumba ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, kabla ya kuvunjwa na yeye akiwa ndani ya nyumba hiyo baada ya kutuhumiwa na wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya kujihusisha na imani za kishirikina.
 Wananchi wenye hasira kali wakivunja nyumba ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, jana siku ya jumapili, baada ya kutuhumiwa na wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya kujihusisha na Imani za kishirikina.
 Wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya wakimzingira Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, kabla ya kumdondoshea kichapo wakimtuhumu kujihusisha na imani za kishirikina.
Wananchi wenye hasira kali wakiendelea kuvunja nyumba ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, jana siku ya jumapili, ambapo akina mama nao hawakukaa nyumba kushiriki tukio hili, baada ya kutuhumiwa na wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya kujihusisha na Imani za kishirikina.
 Baada ya kupingwa  Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, jana siku ya jumapili, Jeshi la polisi lilifanikiwa kufika eneo la tukio  na kumchukua mzee huyo na kumpeleka Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini Mbeya. Pichani ni baadhi ya askali na raia wema wakimuchukua mzee huyo na kumpeleka kwenye gari la polisi kabla ya kumkimbiza hospitali.
 Mke wa Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, katikati akilia kwa uchungu na kupewa msaada na wanawake wenzake, baada ya mumewe kudondoshewa kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti, kata ya Iyunga jijini Mbeya jana siku ya jumapili wakimtuhumu kujihusisha na imani za kishirikina.(Picha na habari na Ezekiel Kamanga)

HITIMISHO
Maoni ya mtandao Jeshi la polisi linapaswa kufika kwa wakati muafaka mara baada ya kupewa taarifa, lakini pia elimu itolewe kwa wananchi kutojichukulia sheria mikononi kwani tuhuma na sio uthibitisho, kwani mahakama pekee ndio ina mamlaka ya kutoa hukumu.

WATUHUMIWA WATATU WA KUMILIKI NOTI BANDIA ZENYE THAMANI YA SHILINGI MIL 559,000/= WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA MARA YA PILI KATIKA MAHAKAMA YA MKOA WA MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:05 | 0 comments
Na mwandishi wetu
Watu wa tatu wakazi wa Uyole jijini Mbeya wamepandishwa kizimbani kwa mara ya pili jana katika mahakama ya mkoa wa Mbeya, kusomewa shtaka la kumiliki noti bandia zenye thamani ya shilingi milioni tano, laki tano na elfu hamsini na tisa.

Akisoma kesi hiyo mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya Mkoa Mbeya mheshimiwa Fransis Kisheny na  mwanasheria wa serikali Grifin Mwakapeje amesema mnamo Novemba 17, mwaka huu  Emmanuel Mwandugule na Faraja Mwakibanza walikutwa na noti bandia zenye thamani ya  shilingi milioni tano na elfu tisa zilizo na namba mbili Noti zenye namba 142 BN 49393 na 268 BN 7949398.

Hata hivyo inadaiwa watuhumiwa hao walikimbia baada ya kuachiwa kwa dhamana katika kesi iliyosomwa Novemba 16, mwaka huu na hivyo kukamatwa tena.

Watuumiwa hao wamekana kosa la kutoroka, hali ambayo imemlazimu hakimu Fransis Kisheny kihairisha kesi hiyo hadi Novemba 30 mwaka huu na hivyo watuhumiwa kupelekwa rumande kwa kuhofia kutoroka tena.

BAADA YA NYUMBA YAKE KUTEKETEZWA KWA MOTO KUTOKANA NA KUJIHUSISHA NA IMANI ZA KISHIRIKINA, MWENYEKITI WA MTAA AHAMIA MTAA WA PILI KWA DADA YAKE NAKO AFUATWA NA SAMANI ZAKE KUTEKETEZWA MOTO NA WANANCHI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:00 | 0 comments
 Vyombo na samani za aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Igoma A, kata ya Isanga jijini Mbeya Bwana Juma Kahawa vilitolewa nje hapo jana kabla ya wananchi wa Igoma B nyumbani kwa dada yake Bi Mary James mwenye umri wa miaka 50 ambaye pia ni balozi wa mtaa huo, ambako Bwana Kahawa amehamia ndipo wananchi wa mtaa huo kuamua kuviteketeza kwa moto kwa madai kuwa hawamtaki Bwana Kahawa kuhamia mtaani kwao kutokana na kujihusisha na imani za kishrikina.
Umati wa wananchi wa mtaa wa Igoma B kata ya Isanga jijini Mbeya uliofika kushuhudia uteketezwaji wa vyombo na samani za aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Igoma A, Bwana Juma Kahawa ambaye amehamia  nyumbani kwa dada yake Bi Mary James mwenye umri wa miaka 50 ambaye pia ni balozi wa mtaa huo, ndipo wananchi wa mtaa wa Igoma B kuamua kuviteketeza kwa moto kwa madai kuwa hawamtaki Bwana Kahawa kuhamia mtaani kwao kutokana na kujihusisha na imani za kishrikina.
Balozi wa mtaa wa Igoma B, kata ya Isanga jijini Mbeya Bi Mary James ahamini kilichotokea baada ya samani zikiwemo zake na za kaka yake Bwana Juma Kahawa kutolewa nje na kuteketezwa kwa moto na wananchi wa mtaa huo kutokana na madai kuwa hawamtaki Bwana Kahawa aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa ya Igoma A anayetuhumiwa kujihusisha na imani za kishirikina.
 Umati wa wananchi wa mtaa wa Igoma B kata ya Isanga jijini Mbeya ukishuhudia uteketezwaji wa vyombo na samani za aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Igoma A, Bwana Juma Kahawa ambaye amehamia  nyumbani kwa dada yake Bi Mary James mwenye umri wa miaka 50 ambaye pia ni balozi wa mtaa huo, ndipo wananchi wa mtaa wa Igoma B kuamua kuviteketeza kwa moto kwa madai kuwa hawamtaki Bwana Kahawa kuhamia mtaani kwao kutokana na kujihusisha na imani za kishrikina.
Mtuhumiwa wa imani za kishirikiana Bwana Juma Kahawa, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Igoma A. Pichani kushoto ni siku ya mwili wa marehemu Ivon Mwakyusa ulipopatikana Novemba 21, mwaka huu, ambapo alipigiwa kura za maoni na wananchi wa mtaa wake wa Igoma A, kwa madai kuwa anajihusisha na imani za kishirikina na lawama zote kubebeshwa yeye kutokana na watoto wa mtaa huo kupotea na kufariki katika mazingira ya kutatanisha.(Picha na Kamanga na matukio, Mbeya Yetu na Chimbuko Letu)

Hitimisho:- Hata hivyo Mwenyekiti wa mtaa wa Igoma B ambako Bwana Juma Kahawa kahamia, Bwana Zacharia Vungwa amesema anasikitishwa na tabia ya balozi wa mtaa huo Bi Mary James kumpokea na kumuhifadhi mtuhumiwa wa imani za kishirikina pasipo kutoa taarifa za kuhamia kwake katika ofisi za serikali za mtaa, na hali inayotishia kuvunjika kwa amani na utulivu mtaani kwake.

MKURUGENZI NA MEYA JIJI LA MBEYA KUCHUKULIWA HATUA KISA, KUWA VINARA WA VURUGU ZA MWANJELWA NA KUMSINGIZIA KANDORO.

Kamanga na Matukio | 05:56 | 0 comments

MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO

* N i kutokana na kupimana nguvu za maamuzi

Na, Gordon Kalulunga, Mbeya
Maaskofu,Wachungaji na wanataaluma mkoani Mbeya wametoa tamko la kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, kuwachukulia hatua za kinidhamu Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga na Mkurugenzi wa Jiji hilo Juma  Idd kutokana na kuwa chanzo cha vurugu zilizotokea jijini hapa hivi karibuni

Tamko hilo limetolewa leo katika Kongamano la kujenga mkakati wa maendeleo ya Mkoa wa Mbeya ambalo liilifanyika katika ukumbi wa Kanisa la Winners lililopo jijini hapa kutoka makanisa yote yaliyopo mkoani Mbeya ambalo Mkuu wa Mkoa alikuwa mgeni rasmi.

Mchungaji William Mwamalanga, ambaye pia ni Mkurugenizi wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya kuhifadhi Mazingira mkoani Mbeya (MRECA) alisema maaskofu na wachungaji wanasikitishwa na vurugu zilizotokea eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya na kwamba hata  Meya na Mkurugenzi wa Jiji wachukuliwe hatua za kinidhami kutokana na kuwa chanzo cha vurugu hizo.

Alisema ''Vurugu zilizotokea haikuwa ni siasa bali ni maamuzi mabaya yaliyofanywa na viongozi waAndamizi wa Jiji la Mbeya katika kushughulikia tatizo la wamachinga wanaouza bidhaa zao eneo la Mwanjelwa''
“Tukiwa na uongozi wa uongo  jiji halitasonga mbele kimaendeleo, vurugu zilizotokea kimsingi pale siyo siasa bali ni maamuzi mabaya ya baadhi ya watu, “alisema Mwamalange huku akishangiliwa na mamia ya viongozi wa dini walioshiriki kongamano hilo.

Alisema maaskofu na wachungaji wanasikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu kumsingizia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Kandoro kwamba yeye alikuwa ndiye chanzo cha vurugu hizo wakati siku ya tukio alikuwa katika ziara wilayani Mbozi kukagua miradi ya maendeleo.

Mchungaji Mwamalanga alisema kimsingi viongozi wa Jiji la Mbeya hasa Meya na Mkurugenzi hawawezi wakakwepa katika suala la vurugu za Mwanjelwa kwasababu walikiwa na nafasi ya kuzungumza na wamachinga kwa utaratibu ambao usingezua vurugu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema anashangaa na baadhi ya watu wanaomsingizia kwamba alishiriki kuchochea vurugu za wamachinga wakati siku vurugu zinatokea alikuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani Mbozi na kwamba Serikali inawatambua wamachinga kama sehemu ya jamii na haiko tayari kukaa nao mbali na katika soko linalojengwa Mwanjelwa watapata nafasi.

Kandoro alisema tangu ateuliwa hajawahi kumwagiza mtu au kiongozi yeyote wa Jiji la Mbeya achukue hatua yeyote dhidi ya wamachinga na kusababisha kutokea vurugu.
“Sijawahi kumwagiza mtu achukue hatua yeyote iliyosababisha vurugu na kimsingi sina sababu maana kwanza ilikuwa ni mapema mno kuchukua maamuzi hayo maana sisi wageni unapofika katika mkoa unahitaji kwanza kusoma mkoa na siyo ghafla unaanza kuchukua hatua,”alisema Kandoro

Kandoro alisema hata hivyo Halmashauri ya Jiji la Mbeya ipo katika mpango wa kuweka utaratibu mzuri wa kuwafanya wamachinga kufanya biashara zao.

Aliongeza kuwa kinachotakiwa ni kuwajengea mazingira wamachinga kufanya biashara zao na pia kufufua viwanda vilivyosimama uzalishaji ili waweze kupata ajira katika viwanda hivyo.

Tamko hilo limekuja wiki moja tu tangu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kilipotoa tamko la  kuchukua maamuzi magumu ya kuwachukulia hatua kali za kinidhamu viongozi wandamizi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya walioshindwa kutimiza wajibu wao na kupelekea kutokea kwa vurugu zilizozua mapambana kati ya wamachinga na polisi jijini hapa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Nawab Mullah alitoa tamho hilo tamko hilo kwa kusema kuwa CCM haiwezi kuacha viongozi wachache ndani ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya wawe chanzo cha vurugu hizo na kusababisha kuvunjia kwa amani kwa maslahi yao binafsi na kupelekea  wananchi kuilaumu serikali ya CCM.

“Kutokana na vurugu za Mwanjelwa CCM baada ya kutafakari kwa kina suala hili na kufanya utafiti wake wa jinsi vurugu zilivyokea na wananchi wa ndani na nje ya mkoa wanavyolizungumzia kimeazimia kuchukua hatu kali kwa viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya walioshinda kutimiza wajibu wao,”alisema Mullah katika tamko hilo.

Mullah alisema CCM ni chama makini ambacho kinawajali na kuwapenda wananchi wake kwa hiyo italazimika kuchukua maamuzi hayo magumu kwa kuhakikisha wale wote wanaoharibu sifa ya Jiji la Mbeya wanaondolewa ili kurejesha imani ya wananchi kwa jiji na serikali ya CCM.

Alisema  wananchi lazima watambue kuwa vurugu ni kama mvua zinanyesha na kuleta mafuriko ambayo huleta madhara makubwa kwa kusomba kila kitu ambapo nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Libya,Misri na Somalia zimeingia katika machafuko ya vita ambayo chanzo chake ni baadhi ya vyama vya siasa kutaka madaraka kwa nguvu kwa kuwashinikiza wananchi kufanya maandamano na vurugu.

Mullah alisema kwa kuwa CCM na serikali yake vipo makini kitaendelea kudumisha amani ya nchi hasa kwa kutambua kuwa hakuna nchi dunia iliyofanikiwa kujenga amani kwa kuvurugu hivyo wanaokuwa chanzo cha kutaka kuvunjika kwa amani watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Vurugu hizo za wamachinga waliokuwa wakipinga kuhamishwa maneeo yao ya kufanyiwa biashara zilianza tangu Novemba 11 mwaka huu na kudumu kwa takribani siku tatu zilisababisha kifo cha mtu mmoja, watu 17 kujeruhiwa kati yao watano kwa kupigwa risasi za moto ambapo polisi walifanikiwa kuwatia mbaroni watu zaidi ya 300 wanaosadikika kushiriki katika vurugu hizo.

Hata hivyo wamachinga hao walisitisha mapambano hayo ambayo pia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lililazimika kuingilia kati baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi kuwasili mjini hapa akitokea mkoani Dodoma ambako alikuwa akihudhuria vikao vya bunge na kuwaomba kusitisha vurugu ambapo walimsikiliza na kuacha kuendelea na vurugu.

WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA DHANDHO WACHAPANA KAVUKAVU BAADA YA KUDHURUMIANA UJIRA WA SHILINGI ELFU MOJA.

Kamanga na Matukio | 05:44 | 0 comments
 Wafanyakazi wa DHANDHO eneo la Kadege jijini Mbeya wakipigana makonde ndani ya kampuni hiyo baada ya kudhurumiana malipo ya ujira shilingi elfu moja, Licha ya sakali kuwepo alishindwa kuchua hatua ya kudhibiti na mpaka pale wafanyakazi wengine walivyoingilia kati kudhibiti ugomvi huo.

Mtandao huu umeshuhudia vijana hao hao wakidundana kwa siku mbili mfululizo, bila uongozi wa kampuni hiyo kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yao. Je, kampuni hii itakuwa na tija?!

WAJASIRIAMALI KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUANZIA NOVEMBA 28, MWAKA HUU MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:31 | 0 comments
 Wajasiriamali mkoani Mbeya kunufaika na mafunzo ya siku tatu ya ujasiriamali yatakayotolewa na kampuni ya Dimod Integrated Solution and Awareness kuanzia siku ya Jumatatu Novemba 28 hadi Novemba 30, mwaka huu siku ya Jumatano, Pichani ni gari ya matangazo ya kampuni hiyo likiwa eneo la Kadege jijini Mbeya jana likitoa matangazo ya mafunzo hayo  yatakayotolewa katika Ukumbi wa Mkapa jijini hapa.
Kampuni inatotoa mafunzo ya ujasiriamali Tanzania ya Dimod Integrated Solution and Awareness , sasa ipo jijini Mbeya kwa ajili ya semina itakayoendeshwa kwa siku tatau kuanzia jumatatu Novemba 28, mwaka huu.

Mafunzo yatakayotolewa na kampuni hiyo ni pamoja na utengenezaji wa Sabuni ya unga, sabuni ya miche, sabuni ya magadi, sabuni za kuogea, sabuni ya majivu, sabuni za maji, shampoo aina zote, mishumaa aina yote, mafuta ya kupakaa, Lotion, maji ya betri, tomato sourcw, chili source, unga wa lishe, wine aina zote, encubeter, biogas, air fresher, bleach, skin scrub, peanut butter, mango pickle, carpet cleaner, window cleaner, tiles cleaner, stain remover na uyoga.

Masomo ya mifugo na biashara , kutengeneza vyakula vya mifugo na ufugaji bora. Semina itafanyika katika ukumbi wa Benjamini Mkapa Conference Center. Fomu shilingi 2,000 na ada ya mafunzo ni shilingi 10,000 kwa masomo yote ya nadharia na vitendo kuanzia majira ya saa 3 kamili asubuhi mpaka saa 8:30 mchana. 

Wakufunzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Dr Didas Lunyungu na Bwana Mohammed Omary ambaye ni Mkurugenzi wa mafunzo na kesho wanatarajia kukutana na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama majira ya saa mbili asubuhi kujadili mambo mbalimbali namna ya kuwawezesha wakazi wa mkoa wa Mbeya kunufaika kibiashara.na uchumi.

ABIRIA 25 WANUSURIKA KATIKA AJALI MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:23 | 0 comments
 Baadhi ya majeruhi akiwemo Bi Philomena Fredy (aliyeketi chini) mara baada ya kutoka ndani ya gari ya abiria aina ya Costa yenye nambari za T 621 BQH wakisubiri msaada wa kwenda Hospitali kupewa huduma ya kwanza baada ya gari yao kugongana na gari ya mizigo aina ya Scania yenye nambari za usajili T 783 ATQ eneo la Kalasha wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya jana majira ya saa moja usiku.
 Mmoja wa abiria akitoa mizigo yake ndani gari ya abiria aina ya Costa yenye nambari za T 621 BQH baada ya gari yao kugongana na gari ya mizigo aina ya Scania yenye nambari za usajili T 783 ATQ eneo la Kalasha wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya jana majira ya saa moja usiku.
 Askari wa Jeshi la polisi akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa abiria wakati wakisubiri kupelekwa Hospitalini mara baada ya kutokea kwa ajali baina ya  gari ya abiria aina ya Costa yenye nambari za T 621 BQH kugongana na gari ya mizigo aina ya Scania yenye nambari za usajili T 783 ATQ eneo la Kalasha wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya jana majira ya saa moja usiku.
 Gari ya mizigo aina ya Scania yenye nambari za usajili T 783 ATQ iliyosababisha ajali kwa kugongana na gari ya abiria aina ya Costa yenye nambari za usajili T 621 BQH eneo la Kalasha wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya jana majira ya saa moja usiku.
***** 
Na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Watu ishirini na tano wamenusurika kufariki dunia kufuatia ajali iliyotokea jana majira ya saa moja usiku eneo la Karasha wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya baada ya kugongana kwa magari mawili ilikiwemo gari la abiria aina ya Costa yenyenambari za usajili T 621 BQH na gari ya mizigo aina ya Scania yenye nambari za usajili T 783 ATQ.

Mtandao huu umeweza kushuhudia ajali hiyo ambapo gari ya mizingo ilikuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye Egno Ignas mwenye umri wa mika 27 mkazi wa Makambako likitokea Mji mdogo wa Tunduma lilionekana kuyumba barabarani na hivyo kupoteza mwelekeo wa dereva wa Costa aliyekuwa katika hali ya mwendokasi nayo ikitokea Tunduma, ambapo dereva wa Costa alipojaribu kulikwepa gari la mizigo na kuligonga kwa mbele hali iliyosababisha costa kupoteza mwelekeo na kuupalamia mashamba.

Akizungumza na mtandao huu mmoja wa abiria Bi Philomena Fredy amesema gari ya mizigo ilikuwa mbele yao na dereva alipojaribu kulikwepa abiria wakasikia kishindo kikubwa na kufumba na kufumbua wakashituka gari lao la abiria lipo pembezoni mwa barabara baada ya kuparamia matuta.

Majeruhi wote walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na wengine katika hospitali ya Mbozi Mission inayomilikiwa na kanisa la Moraviani Jimbo la Kusini Magharibi.

Hata hivyo polisi walifanikiwa kufika mapema eneo la tukio na kuchukua maelezo ya Utingo wa gari ya mizigo Bwana Godi Mlingo mwenye umri wa miaka 21 ambapo alisema gari yao ilizima ghafla na kupoteza mwelekeo.

GARI LILILOIBIWA NYUMBANI KWA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA BABLO YAKAMATWA JIJINI MBEYA NA JESHI LA POLISI.

Kamanga na Matukio | 04:50 | 0 comments
Jeshi la polisi mkoani Mbeya limefanikiwa kukamata gari iliyoibiwa kitongoji cha Ichenjezya wilayani Mbozi yenye nambari za usajili T 669 DCK aina ya Toyota Prado inayomilikiwa na Kampuni ya Bablo yenye makao makuu wilayani humo mkoani humo na kukamatwa jijini Mbeya.

Gari hiyo iliibiwa majira ya saa tano asubuhi Novemba 23, mwaka huu, nyumbani kwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo ambapo ndani ya gari kulikuwa na watoto wawili ambao walitelekezwa njiani.

Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la ujambazi na kwama watu wawili wanashikiliwa na Jeshi hilo la polisi.

 Hata hivyo imedaiwa kuwa hilo ni tukio la pili kutokea ambapo la kwanza lilitokea Novemba 21, mwaka huu wilayani Mbozi ambalo nalo lilikamatwa eneo la Mlowo wilayani humo.

WANANCHI WACHOMA MOTO NYUMBA MBILI YA MWENYEKITI WA MTAA NA MGANGA KWA KILE KINACHODAIWA KUJIHUSISHA NA IMANI ZA KISHIRIKINA MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 02:56 | 0 comments
 Wananchi wa mtaa Ilolo Igoma A Kata ya Isanga  jana mchana wamezichoma moto na kuzivunja Nyumba mbili ya Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana  Juma Kahawa na ya Mganga Mfipa kufuatia tamko la wananchi kuwataka wahame kwa kile kinachodaiwa kujihusisha na imani za kishirikina.
 Wananchi na wanafunzi wakiwa eneo la tukio ambapo wananchi hao jana mchana kuzicho moto na kuzivunja Nyumba mbili ya Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana  Juma Kahawa na ya Mganga Mfipa kufuatia tamko la wananchi kuwataka wahame kwa kile kinachodaiwa kujihusisha na imani za kishirikina.
 Pichani ni mabati yaliyoteketea kufuatia sakata la Wananchi wa mtaa Ilolo Igoma A Kata ya Isanga  jana mchana wamezichoma moto na kuzivunja Nyumba mbili ya Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana  Juma Kahawa na ya Mganga Mfipa kufuatia tamko la wananchi kuwataka wahame kwa kile kinachodaiwa kujihusisha na imani za kishirikina.
 Vikosi vya zima moto na askali polisi wakiwa eneo la tukio jana kudhibiti moto na wananchi kutoendelea kuvunja nyumba Nyumba mbili ya Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana  Juma Kahawa na ya Mganga Mfipa kufuatia tamko la wananchi kuwataka wahame kwa kile kinachodaiwa kujihusisha na imani za kishirikina.
 Moja ya sehemu zilizobomolewa na kuchomwa moto na wananchi wa mtaa Ilolo Igoma A Kata ya Isanga  jana mchana katika Nyumba mbili ya Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana  Juma Kahawa na ya Mganga Mfipa kufuatia tamko la wananchi kuwataka wahame kwa kile kinachodaiwa kujihusisha na imani za kishirikina.
 *****
Na mwandishi wetu.
Wananchi wa mtaa Ilolo Igoma A Kata ya Isanga  jana mchana wamezichoma moto Nyumba mbili ya Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana  Juma Kahawa na ya Mganga Mfipa kufuatia tamko la wananchi kuwataka wahame kwa kile kinachodaiwa kujihusisha na imani za kishirikina.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya wananchi waliitisha mkutano leo kujadili chanzo cha tukio lakini ukaahirishwa kufuatia kutokuwepo kwa ulinzi toka  jeshi la polisi ambao wangeweza kuzuia lolote mkutanoni hapo.

Baada ya wananchi hao kuelezwa kuwa hapatakuwepo mkutano huo walipandwa na hasira na kujichukuliwa sheria mikononi mwao kwa kuzichoma nyumba ya Juma Kahawa ambaye alipigiwa kura 150 na ile ya Mganga Mfipa aliyepigiwa kura 20.

Vikosi vya  Zima moto na Jeshi la Polisi vilifika eneo la tukio na kuthibiti  moto uliokuwa ukiendelea kuteketea nyumba hizo.

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA NYUMBA ALIYOKUWA AKIISHI KUCHOMWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 02:54 | 0 comments
 Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi.
*****
Na mwandishi wetu
 Mkazi mmoja wa Mbambo wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya Lastoni Mwangosi anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 40 hadi 50 amefariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kuchomwa moto na watu wasiofahamika.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema Bwana Mwangosi amefikwa na mauti jana majira ya saa 1 usiku baada ya nyumba yake kuchomwa moto.

Hata hivyo Kamanda Nyombi amemaliza kwa kusema  chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina na Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini aliyehusika na tukio hilo .

DALADALA YA ITV YAFANA MKOANI MBEYA KUPITIA ZIARA YAO.

Kamanga na Matukio | 05:25 | 0 comments
Wanachuo wa TIA Mbeya wakiingia katika Daladala, inayomilikiwa na kituo cha televisheni cha ITV katika ziara yao mkoani Mbeya hapo jana, ambapo wanavyuo hao walipata fursa ya kuweza kuchangia maoni yao kupiti mada zinazoendeshwa na kipindi cha Daladala kinachorushwa ITV kila siku kuanzia saa Kumi na mbili na nusu jioni hadi saa moja kamili usiku na watangazaji wawili Bi Kiroboto na Bwana Daniel Kijo. 
Mtangazaji wa Kipindi cha Daladala kinachorushwa kila siku kuanzia Saa kumi na mbili na nusu hadi saa moja kamili usiku kupitia Televisheni ya ITV Bi Kiroboto akiwa ameketi katika kiti cha daladala wakati wa ziara yao mkoani Mbeya hapo jana.
Mtangazaji wa Kipindi cha Daladala kinachorushwa kila siku kuanzia Saa kumi na mbili na nusu hadi saa moja kamili usiku kupitia Televisheni ya ITV Bwana Daniel Kijo akiandikisha majina ya washiriki watakaongia maoni katika mada zinazoendeshwa na kipindi hicho, katika ziara yao mkoani Mbeya hapo jana.

BI ROSE MUHANDO AVURUGA MKUTANO WA INJILI KWA KUTOKUFIKA, LICHA YA KULIPWA MILIONI 2.5 MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:05 | 0 comments
Baada ya kupewa mwaliko wa kutoa huduma ya neno la Mungu katika mkutano wa Injili  mkoani Mbeya na kushindwa kufika kwa Mwimbaji wa nyimbo za Injili Bi Rose Muhando, Pichani juu ni Bwana Riziki Mwakapugi akionesha stakabadhi za malipo ya benki(Pay in slip) ya shilingi milioni mbili nalaki tano zilizotumwa kwenye akaunti ya Mwimbaji huyo, kupitia benki ya Barclays. Mkutano huo wa injili ulioanza Novemba 18 hadi 20, mwaka huu  uliandaliwa na kanisa la Bethel Miracle Centre(BMC), Kituo cha Mbinguni lililopo eneo la Soweto jijini Mbeya.
 Jengo la Kanisa la Bethel Miracle Centre(BMC), Kituo cha Mbinguni lililopo eneo la Soweto jijini Mbeya, ambalo lilitoa mwaliko kwa Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Bi. Rose Muhando, na kushindwa kufika licha ya kulipwa fedha taslimu shilingi milioni Mbili na nusu alizokuwa akizihitaji ili aweze kuhudhuria.
 Moja ya mabango yaliyotapakaa jiji zima likionesha muda, siku na mahali Mkutano wa injili utakapofanyika pamoja na wasanii wa nyimbo za Injili watakaotoa huduma ya neno la Mungu kupitia uimbaji, akiwemo Bi Rose Muhando, ambaye hakuweza kufika licha ya kuingiziwa kwenye akaunti yake shilingi milioni mbili na nusu alizokuwa akizihitaji ili aweze kuhudhuria.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger